Header Ads Widget

JIMBO LA MUSOMA MJINI YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MIAKA 4 YA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN

                  Na Shomari Binda-Musoma 

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amezungumzia miaka 4 ya uongozi wa Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan na maendeleo yaliyofikiwa.

Akizungumza kwa njia ya simu na Matukio Daima leo machi  19,2025 ikiwa ni miaka 4 kamili ya uongozi huo amesema yapo ya kujivunia na yanayoonekana ikiwemo miradi ya maendeleo ndani ya jimbo la Musoma mjini 

Mathayo ameanza kwa kuzungumzia miradi ya elimu kwa kuelezea namna shule mpya za msingi na sekondari zilivyojengwa ndani ya jimbo kwa maendeleo ya elimu.

Amesema kwenye Kata za Bweri,Buhare,Makoko na Kigera zimejengwa shule mpya na za kisasa na maeneo mengine kuongezwa madarasa ambayo imekuwa chachu ya elimu.

Mbunge huyo amesema kumsaidia mtoto wa kitanzania na wa jimbo la Musoma mjini ni kumpa elimu na hilo limefanyika kupitia serikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan 

" Tunapozungumzia miaka 4 ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tunazungumzia mafanikio yaliyopatikana kwa taifa zima na jimbo letu la Musoma mjini.

" Kwenye upande wa elimu pekee kwa kipindi hiki cha miaka 4 tumepokea fedha nyingi ambazo zimejenga shule mpya za msingi na sekondari za kisasa na leo watoto wetu wanasoma sehemu nzuri kwa kweli tunamshukuru Mama Samia",amesema.


Amesema licha ya eneo hilo la elimu sekta ya afya,maji na miundombinu imefìkiwa ndani ya jimbo la Musoma mjini na hakuna shida kwenye maeneo hayo.

Akizungumzia miradi ya kimkakati mbunge Mathayo  amesema ndani ya jimbo la Musoma tayari mradi wa soko la kisasa la Nyasho ujenzi wake utaanza hivi karibuni baada ya kupatikana kwa mkandarasi pamoja na stendi ya kisasa ya mabasi ya Bweri.

Mbunge huyo wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameendelea kumshuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa miradi ya maendeleo na kudai hawana deni naye bali anacho wadai ni kumchagua kwa kura nyingi kwenye uchaguzi wa mwaka 2025

Leo machi 19,2025 Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametimiza miaka 4 madarakani baada ya kifo cha Rais wa awamu ya 5 Rais Dkt.John Pombe


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI