Na. Kwiyeyu Singu
Katika sehemu hii, uchambuzi wangu utaangazia masuala ya kiutawala na kiuchumi.
Kiutawala:
Nzega ni Wilaya kongwe, ina Halamashauri mbili, yaani Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Mji, Halamashauri hizi zinaundwa na Tarafa nne ambazo ni Tarafa ya Mwakalundi, Tarafa ya Bukene, Tarafa ya Puge, na Tarafa ya Nyasa.
Tarafa zote hizi zina kata 46.
Jimbo la Bukene ndilo lenye Tarafa mbili ya Mwakalundi na Bukene yenyewe.
Hivyo, Wilaya ya Nzega ni eneo la kiutawala tangu enzi za ukoloni, lililojumuisha Kahama kabla haijawa Wilaya, Igunga kabla haijawa Wilaya na kwa kiasi fulani eneo la Shinyanga Mjini.
Na kufikia mwaka 2014, Nzega ilipitishwa kuwa Mkoa wa Nzega ikiwa na wilaya tano, yaani Bukene, Manonga, Igunga, Nzega na Puge, hivyo kilichokuwa kimesubiliwa ni miundombinu tu ya kiutawala kukamilika ili itangazwe rasmi.
Kiuchumi:
Jimbo la Bukene linazalisha mazao makuu mawili ambayo ni zao la mpunga na zao la mahindi, inagwa vile vile panalimwa mazao mengine kama karanga na mihogo, kuna kilimo cha matunda na mbogamboga pia kwa kiasi fulani.
Jimbo la Bukene ndilo linalotegemewa kwa asilimia kubwa ktk mahitaji ya sokoni kwa maana ya mbogamboga, matunda na hata mazao ya chakula yenyewe (yaani mahindi na mpunga).
Mazao mengine ya kibiashara kama Pamba, Tumbaku na Alizeti yalitiliwa mkazo miaka ya 90 lakini sasa hayalimwi tena.
Ardhi iliyopo ktk Jimbo hili haipishani sana na ardhi iliyopo ktk majimbo mengine ya Nzega Mjini na Nzega vijijini, kwa kiasi kikubwa ardhi inakubali sana kwa mazao ya mpunga, karanga, mahindi, mihogo, alizeti, pamba, vitunguu, matunda kama machungwa na rimao, ndizi, korosho, ndizi, matikiti, matango, kabechi, chainizi, pilipili, matole, hoho, na mbogamboga zote.
Kutokana na ubora huo wa ardhi, pia ufugaji wa mifungo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, samaki na hata kuku unakubalika.
Pia kuna mapori ingawa yamevunwa sana na watu wasiokuwa na nia njema wakiwemo wanasiasa waliosafirisha mbao, lakini yanaweza kufungiwa nyuki.
Pamoja na sifa na ubora wote huo ktk jimbo la Bukene lakini bado linakabiliwa na changamoto nyingi.
Kwanza wananchi wengi ni maskini wa kipato na elimu, ingawa suala la elimu duni ni janga la kitaifa, lakini yapo maeneo kama ya Nzega suala la elimu halipewi nasafi ya mbele au kipaumbele.
Hili ni tatizo linaloikumba zaidi jamii ya Nzega pengine kuliko kwingineko, tatizo hili limechangiwa zaidi na wanasiasa kutojali umuhimu wa sekta hii kama sehemu muhimu ya kumkwamua mtu maskini.
Hata hivyo, wanasiasa wameyapa mgongo maendeleo ya wananchi, si madiwani wala mbunge, maeneo ya kimkakati ambayo yalitarajiwa kuwa na maendeleo makubwa, mpaka sasa yamebaki kuwa duni.
Kwa mfano, kata ya Bukene, Itobo, Mwangoye, Mwamala, Mambali, mpaka sasa yamebaki kuwa historia tu ya makazi ya waarabu, wenyeji (kwa kuongozwa na wanasiasa wao) hawaonyeshi kupaendeleza kabisa licha ya maeneo haya kuwa yamezungukwa na fursa nyingi za kiuchumi.
Kata ya Bukene imezungukwa na kata zenye ardhi nzuri ya mpunga, mahindi na mazao mengine, Mwamala nayo imezungukwa na kata zenye ardhi nzuri ya mpunga na mahindi na mazao mengine, halikadhalika Itobo na Mwangoye.
Zipo sababu na changamoto ambazo zimechangia maeneo haya ya kimkakati kutoendelezwa na kubaki yamedumaa mpaka leo.
Moja wapo wa sababu na changamoto hizo ni hizo nilizozitaja hapo juu, yaani:
(i) Elimu duni ya wakazi au wananchi wa maeneo husika,
(ii) Athari za kitamaduni hasa utamaduni wa kiaarabu waliokaa maeneo hayo,
(iii) Kukosekana kwa siasa safi. Shida hii sio kwa jimbo la Bukene tu, bali majimbo yote ya Nzega kama si na maeneo mengine mengi, watu wengi wamekuwa wakijiingiza kwenye siasa wakiwa hawayajui majukumu ya uongozi wa kisiasa, hata wanapokuwa ktk nafasi hizo hawajishughulishi kuyajua majukumu hayo, nafasi hiyo wanaitumia kama fursa ya kujitajilisha kwa kufanya ufisadi badala ya kufanya jitihada za kuleta maendeleo kwa wananchi.
Eneo hili la siasa nitalizungumuzia zaidi kwenye makala itakayofuatia kwa mapana zaidi, kwa sababu tumezunguka ktk kata zote za Wilaya ya Nzega kufanya utafiti wa kawaida ktk nyanja hizi za kiuchumi, kisiasa na kitamaduni na kubaini mambo kadhaa ambayo tutayaweka wazi kwa faida ya jamii ya Nzega na taifa letu.
Makala ijayo itaangazia zaidi masuala mawili, yaani nyanja ya kisiasa na utamaduni wetu, kwa kuanzia na vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa tangu mwishoni mwa ubunge wa mzee Kahumbi wakati anamkabidhi kijiti Tedy Kaselabantu aliyekuwa UDP kisha kuhamia CCM.
Wakati huo Chama cha Mapinduzi ndipo kilianza kukabiliwa zaidi na vyama vya upinzani.
Nitumie nafasi hii na kwa mara nyingine kuwakaribisha wana Nzega na wadau wengine wa maendeleo popote walipo, kuwaalika ktk group la "Mchakato Majimboni" ili kuchangia mawazo na kupendekeza namna bora ya kuiendeleza jamii hii ktk nyanja zote muhimu za kimaendeleo.🙏🏻
Itaendelea....
Mijadala yetu inafanyika ktk group la WhatsApp la "Mchakato majimboni"
Kwiyeya Singu. 0784977072
0 Comments