Na Matukio Daima Media
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa anayewakilisha Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Blastus Mgimwa, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Katibu wa Itikadi, Uenezi, na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makala kujenga Chama na kutoa majibu sahihi kwa wananchi dhidi ya upotoshaji wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kupitia Kampeni yao ya No Reform No Election.
Mgimwa alisema kuwa hotuba na hoja za Amos Makala katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mashujaa mnamo Ijumaa, Machi 28, 2025, zimedhihirisha dhamira ya dhati ya CCM katika kujibu hoja na propaganda zinazotolewa na vyama vya upinzani, hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia kampeni yao ya "No Reform, No Election."
Mgimwa alisema kuwa kampeni hiyo ililenga kupotosha wananchi, lakini hotuba ya Makala ilieleza ukweli na kuwafanya wananchi kuelewa nia njema ya CCM katika kuleta maendeleo ya nchi.
Katika mahojiano yake na Matukio Daima Media, Mgimwa alisema kuwa kupitia mkutano wa Makala, wananchi wengi wameweza kuelewa kuwa CCM inaendelea kuwatumikia wananchi kwa dhati, tofauti na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani.
Alisema kuwa kauli na hoja za Makala zilikuwa na nguvu kubwa ya kuonesha ushindi wa CCM kwa wananchi, jambo ambalo limesababisha kupungua kwa ushawishi wa propaganda za upinzani.
Mbali na kujibu hoja za wapinzani, Amos Makala amepongezwa pia kwa hatua yake ya kuongoza harambee ya kuchangia pesa kiasi Cha Tsh milioni 1.5 mjumbe wa Baraza la Wanawake Taifa kupitia CHADEMA (BAWACHA), Sigrada Mligo aliyejeruhiwa na mlinzi wa makamu mwenyekiti CHADEMA Taifa John Heche kwenye kikao Chao Cha ndani mkoani Njombe.
Kuwa Kitendo kilichofanywa na Makala kimeonyesha kwa vitendo kauli mbiu ya CCM ya "Utu na Kazi." ya CCM .
Mgimwa alieleza kuwa hatua hiyo imethibitisha kuwa CCM ni chama kinachojali ustawi wa jamii bila kujali itikadi za kisiasa, na kwamba mshikamano wa kitaifa ni jambo la kipaumbele kwa chama hicho.
Mgimwa alisisitiza kuwa imani ya wananchi kwa CCM ni kubwa na matarajio yao ni kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anapata ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao.
Alisema kuwa kazi kubwa iliyotekelezwa na serikali ya CCM kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ni sababu kuu inayowafanya wananchi kuendelea kuiamini CCM.
Kwa mujibu wa Mgimwa, miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kote nchini ni kielelezo cha juhudi za CCM za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Kwa upande wa maendeleo, Mgimwa aliainisha kuwa miradi mikubwa ya miundombinu, elimu, afya, na huduma za kijamii imetekelezwa kwa kiwango cha juu chini ya uongozi wa CCM.
Alitoa mifano ya barabara za Lami zimejengwa na Wao wakazi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini wameonja Matunda ya lami ya Mtili Ifwagi , madaraja, vituo vya afya, shule, na huduma za maji safi na salama ambazo zimeimarishwa katika maeneo mengi nchini.
Alisema kuwa mafanikio haya yanatokana na uongozi thabiti wa CCM, ambao unazingatia mahitaji ya wananchi na kuhakikisha maendeleo yanawafikia wote bila ubaguzi.
Mgimwa pia aligusia mafanikio ya CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana, ambapo chama hicho kilipata ushindi wa kishindo.
Alisema kuwa ushindi huo ni ishara ya namna wananchi wanavyoendelea kuiamini CCM na sera zake.
Aliongeza kuwa matumaini ya wananchi ni kuona ushindi kama huo ukijirudia katika uchaguzi mkuu ujao, ili serikali iendelee kutekeleza miradi yake kwa ufanisi zaidi.
Katika kumpongeza Amos Makala, Mgimwa alisisitiza kuwa Makala ni kiongozi mwenye dhamira ya dhati ya kuhakikisha kuwa CCM inabaki kuwa chama chenye nguvu na kinachokubalika kwa wananchi.
Alisema kuwa uwezo wa Makala wa kuwasilisha hoja zenye mantiki, kuwahamasisha wananchi, na kuwaunganisha Watanzania wa makundi mbalimbali ni sifa inayomfanya kuwa kiongozi anayestahili pongezi na kuungwa mkono.
Mgimwa pia alieleza kuwa ushirikiano wa viongozi wa CCM katika kuhakikisha kuwa chama kinazidi kuimarika ni jambo la kujivunia.
Alisema kuwa mshikamano wa viongozi wa chama unachangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya CCM, na kwamba viongozi kama Amos Makala wanapaswa kuungwa mkono ili kuhakikisha kuwa chama kinaendelea kuwa imara.
Mgimwa alitoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kuendelea kukiamini chama na kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama.
Alisema kuwa maendeleo ya Tanzania yanategemea mshikamano wa wananchi na uongozi madhubuti wa CCM.
Pia alihimiza wananchi kutathmini maendeleo yaliyofanywa na serikali ya CCM na kuendelea kukiamini chama kwa ajili ya ustawi wa nchi.
Kuwa Katika muktadha wa siasa za Tanzania, ambapo ushindani wa kisiasa unazidi kuimarika, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuthibitisha uimara wake kupitia viongozi wake makini na wanaotekeleza sera zake kwa vitendo
Kwani alisema Amos Makala ni ishara ya namna viongozi wa CCM wanavyoendelea kuthamini na kutambua juhudi zinazofanywa na wenzao katika kuhakikisha kuwa chama kinabaki kuwa chenye nguvu.
Kupitia hotuba za Makala na hatua zake za kuonesha mshikamano wa kitaifa, CCM inazidi kuthibitisha kuwa ni chama chenye dira na kinachotekeleza sera zake kwa vitendo .
Alisema msingi huo, ni dhahiri kuwa wananchi wataendelea kukiamini CCM na kukipa ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.
0 Comments