Header Ads Widget

BALOZI BATLDA BURIAN AUNGANA NA WAISLAMU WA TANGA KUSHEREKEA EID -AL-FITR, AISISITIZA AMANI NA MSHIKAMANO"

 
Na Ashrack Miraji Matukio Daima App

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, leo ameungana na Waislamu mkoani Tanga kushiriki katika ibada ya Eid-al-Fitr iliyofanyika kwenye Msikiti wa Ijumaa Jijini Tanga. Akizungumza  na waandishi wa habari baada ya ibada, Balozi Burian aliwataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kutenda matendo mema waliyoyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza amani na mshikamano katika jamii.

"Amani ni jambo la muhimu katika jamii yetu. Kama vile tulivyoshuhudia maelewano na upendo miongoni mwa waumini katika mwezi wa Ramadhani, ni jukumu letu sote kuendeleza hali hiyo hata baada ya mfungo. Kwa kupitia matendo yetu ya kila siku, tunaleta Amani na ustawi katika taifa letu," alisema Balozi Burian.

Aliongeza kuwa ni muhimu waumini waendelee kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maisha marefu na Baraka, huku akiwashukuru kwa kushirikiana na Serikali katika kusaidia watoto yatima na wengine wenye mazingira magumu.

"Kwa upande wa Rais Samia, tunamshukuru kwa kutoa sadaka ya mbuzi katika vituo vya watoto yatima, na hii ni ishara ya upendo na mshikamano. Tunaendelea kumuombea kwa maisha marefu na Baraka tele. Amani ya taifa letu inatokana na juhudi za kila mmoja wetu," alisema.

Katika hatua nyingine, Balozi Batilda Burian alikazia suala la uchaguzi mkuu unaoendelea, akisema kuwa ana imani kuwa wakazi wa Tanga na Watanzania kwa ujumla watamchagua kwa kishindo, huku akiwataka kuendelea kuwa na ukarimu na kuenzi amani.

"Uchaguzi huu ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu, lakini tunasisitiza kuwa Amani ni kipaumbele chetu. Tutaendelea kushirikiana na serikali kwa ajili ya maendeleo ya mkoa wetu na taifa kwa ujumla," aliongeza.

Mwisho, Balozi Burian aliwatakia Waislamu mkoani Tanga furaha ya Eid, na kuendelea kufanya matendo mema kwa ajili ya amani ya taifa letu.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI