Header Ads Widget

WANACHAMA WA CCM WAITWA DODOMA

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na watanzania kwa ujumla wamekaribishwa katika kuadhimisha miaka 48 ya Chama hicho sherehe zitakazofanyika jijini Dodoma. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini ,Januari 3,2025 Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA.Amos Makalla amesema kuwa jambo kubwa katika sherehe hizo ni pamoja na Mweyekiti wa Chama hicho ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

“Nitoe wito kwa watanzania wote walioko Dodoma na nje ya Dodoma wana CCM na wasiokuwa wana CCM kufika katika uwanja wa Jamhuri kwa kuwa milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 alfajiri hii siyo ya kupewa kadi kila mtu anakuja,”amesema

pia Chama hicho kinatarajia kuwatambulisha Rasmi wagombea wake katika nafasi ya ngazi ya Urais na Makamo kwa wanachama wake Januari 5,2025 jijini Dodoma.

“Kwa sasa CCM inawatangaza wagombea wao kwa wana CCM na muda ukifika watambulishwa kwa wananchi ili kufanikisha suala la kutimiza masuala ya uchaguzi kikatiba lakini sasa hivi ni muda wa wanachama wa CCM kutambilishwa wagombea wao,”amesema Makalla.

Aidha CPA  Makalla amewataka wana CCM wote kutoka mikoa ya jirani na walioko katika Dodoma kuhakikisha wanafika katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushuhudia sherehe hizo .

Hata hivyo CCM inafanya sherehe yake ya kutimiza miaka 48 tangu kuzaliwa kwake na katika tukio hilo jambo kubwa ni kuwatangaza wagombea ambao walipitishwa na mkutano mkuu kugombea nafasi ya Urais na makamu ya Rais kwa Tanzania bara pamoja na mgombea Urais kwa Tanzania visiwani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI