Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Kagera.
MAHAKAMA kuu Kanda ya Bukoba imetoa Cheti Cha Shukrani (certificate of Appreciation)kwa Matukio Daima Media kutokana na mchango wake mkubwa wa kuhabarisha umma wiki ya sheria nchini .
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe,Immaculata Kajetan Banzi ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya week ( juma) ya sheria ndani ya Mkoa huo alisema leo kuwa kazi kubwa imefanywa na vyombo vya habari hasa Matukio Daima media ambayo imetojilea kurusha Moja kwa Moja Matukio ya wiki ya sheria nchini.
Jaji Immaculata alisema kuwa vyombo vya habari vilivyoshiriki katika juma la sheria ni vingi na vyote vinapongezwa kwa japo kipekee Matukio Daima Media kuwa Media pekee iliyorusha vipindi MUBASHARA (live) katika mada zilizokuwa zikitolewa katika siku tofauti kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya sheria mbalimbali zinazohusu Mahakama.
"Tulitumia Vyombo vingi sana vilivyopo hapa karega na nje ya Kagera ,zilikuwepo radio, Television mbalimbali zikiwemo Tv Mtandao hivyo nawapongeza sana kwa kazi nzuri ya kujitoa kwa moyo safi katika kazi za Mahakama yetu ,amesema Jaji Immaculata "
Alisema kuwa katika juma la sheria mahakama ya Kanda Bukoba wameweza kutoa elimu katika sehemu mbalimbali yakiwemo magereza yote yaliyomo Mkoani humo,wafanya Biashara ,waendesha pikipiki,pamoja na wanafunzi .
0 Comments