Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Katibu Mwenezi wa Baraza la wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Taifa Sigrada Mligo amesema Serikali inatakiwa kuchukua hatua ya kuanza kuchimba Madini yaliyopo kwenye Wilaya za Ludewa na Makete ili Uchumi wa Taifa na wananchi ukue.
Akiwa Iwawa Mjini Makete mkoani Njombe Mligo amesema Madini yaliyopo yanaweza kuwaondoa watanzania kwenye umasikini na miundombinu ya barabara ingejengwa lakini maamuzi ya wananchi kuchagua viongozi wasio na hofu ya mungu wala huruma kwa watanzania ndio sababu iliyowafikisha hapo.
Aidha Mligo amesema michango mingi kwa watoto shuleni inatokana na kuendelea kuwaweka mamlakani viongozi wa Chama Kimoja na wasio na uchungu kwa wananchi wake hivyo wanapaswa kuchukua hatua katika uchaguzi mkuu Ujao.
Medrick Kyando Mwenyekiti Chadema kata ya Iwawa na baadhi ya waliokuwa wagombea nafasi mbalimbali za udiwani na Uenyekiti wa serikali za mitaa wamesema Bado maridhiano yamekuwa yakishindwa kutekelezeka jambo linaloashiria kukwama kwa Demokrasia ndani ya Taifa huku wakisema endapo watapewa ridhaa katika uchaguzi ujao watakwenda kutekeleza miradi iliyokwama kwa miaka mingi ikiwemo Changamoto za bili za maji na barabara.
Veronica Mlonganile ni Mwenyekiti Baraza la wanawake Chadema mkoa wa Njombe ambaye anasema kwa kuwa wanawake Wengi na watoto ndio Wamekuwa waathiriwa wakubwa katika masuala mbalimbali hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu katika siku za usoni ili waje kuwa watetezi wa Wengine.
0 Comments