Header Ads Widget

MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA MASHAMBANI NJOMBE KUANZA SASA

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Tume ya umwagiliaji chini ya wizara ya Kilimo imetiliana saini ya utekelezaji wa mradi wa uchimbaji Visima 30 Katika Halmashauri sita za Mkoa wa Njombe mradi unaokwenda kuwa mkombozi kwa wakulima hasa wanaolima mazao ya muda mrefu yanayotegemea maji wakati wote.

Mhandisi wa Umwagiliaji mkoa wa Njombe Machage Mwema anasema mkataba wa utekelezaji wa mradi huo unaanza mara moja na utakwenda kutekelezwa katika vijiji vyenye mashamba makubwa katika Halmashauri zote sita za mkoa wa Njombe.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Juma Sweda amesema mradi huo utakwenda kuzalisha mamilionea wengi kupitia kilimo huku akionya ubabaishaji katika utekelezaji wa Mradi.

Nestory Mahenge ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe ambaye anasema uchumi wa wananchi na Serikali utakwenda kukua mra dufu baada ya kuanza kufanya kazi mradi huo na hivyo anaishukuru serikali kwa kuona adha ya maji kwa wakulima.

Kwa upande wao wakulima wa parachichi Ngalanga kata ya Mjimwema eneo ambalo litachimbwa kisima wamesema kilio chao kikubwa ni changamoto ya maji kipindi cha kiangazi katika mazao yao hivyo utakuwa muarobaini.


Serikali ilielekeza kuchimbwa kwa visima 150 kwa kila Halmashauri ambapo mkoa wa Njombe unatarajiwa kuchimbiwa visima 900 ikiwa kwa hatua za awali vinaanza vitano na Mkandarasi wa kutekeleza mradi huo Mubaraka Ngwada toka Kampuni ya MNFM Construction anaahidi kufanyakazi hiyo kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI