Header Ads Widget

MIAKA MINNE YA SAMIA ONGEZEKO LA MIRADI KUTOKA NJE YA NCHI




Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima app Dodoma


KUMEKUWEPO na ongezeko la usajili wa miradi kutoka nje linalotokana na juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuitangaza nchi na kuhamasisha uwekezaji kupitia sera  maalum ya mashirikano kupitia Diplomasia ya kiuchumi. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri ameyasema hayo leo wakati akizingumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo tarehe 27 Februari, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.


Amesema ongezeko la miradi linatokana na ushiriki wa Tanzania katika makongamano mbalimbali nje ya Nchi na maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini.


Aidha ameeleza Thamani ya mitaji ya miradi iliyosajiliwa imepanda kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 hadi bilioni 23.67, ishara ya kuongezeka kwa uaminifu wa wawekezaji kwa serikali ya Awamu ya Sita.



"Usajili wa Miradi ya Uwekezaji"

Amesema kuwa katika kipindi mwaka Januari2021 hadi Januari 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi 2,020 ambayo ilikadiriwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa Dola za Marekani bilioni 23.67 na kutoa jumla ya ajira 523,891," Amesema Mkurugenzi huyo Mtendaji na kuongeza kuwa.


"Kati ya miradi hiyo asilimia 35 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya Wageni na asilimia 23.1 ni ya ubia kati ya Watanzania na Wageni, " Amesema


Aidha amesema, tathmini inaonesha kuwa idadi kubwa ya miradi iliyosajiliwa ipo katika sekta za kipaumbele ambazo ni: Uzalishaji viwandani miradi  538 (45.29%), Usafirishaji miradi 225 (18.94%), Utalii miradi 110 (9.26%),  sekta ya ujenzi wa majengo ya biashara miradi 106 (8.92%) Kilimo miradi 106 (8.50%), kama inavyoonesha katika . 


"Mgawanyo wa Umiliki katika Miradi ya Uwekezaji Jan, 2021 hadi Jan, 2025"

Katika miradi hii, asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni, na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni ukilinganisha na miradi iliyosajiliwa katika kipindi cha kuanzia 2017 hadi 2020 ambapo asilimia 27.4 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 44.1 ni ya wageni, na asilimia 28.5 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni.


Juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita kushusha kiwango cha chini cha kuruhusu kusajili mradi Kituo cha Uwekezaji ili kupata vivutio kutoka dola za Marekani laki moja mpaka dola 50,000 kimesaidia kuongeza usajili wa miradi ya wawekezaji wa ndani.


"Thamani ya Mitaji ya Miradi ya Uwekezaji Iliyosajiliwa TIC Kisekta"

Katika kipindi cha Awamu ya Sita, kuanzia Januari 2021 hadi Januari 2025, TIC imesajili miradi 2,020, ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa katika kipindi cha 2017-2020. Thamani ya mitaji ya miradi hii inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 23.67, ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2. Aidha, miradi hii inatarajiwa kutoa ajira 523,891, ongezeko la asilimia 284.6 ukilinganisha na ajira 136,232 za 2017-2020.


"Katika miradi hii, asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni, na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni.


Mafanikio ya Usajili wa Miradi KisektaTathmini inaonesha kuwa idadi kubwa ya miradi iliyosajiliwa ipo katika sekta za kipaumbele ambapo Sekta ya uzalishaji viwandani inaongoza kwa kuwa na jumla ya miradi 917 sawa sawa na asilimia 45.39  ikifuatiwa na Sekta ya Usafirishaji yenye miradi 348 sawa na asilimia 17.22 na kufuatiwa na Sekta ya Ujenzi wa majengo ya biashara 304 sawa asilimia 15.04. Sekta ya nne inayoongoza kufaya vizuri ni sekta ya Utalii yenye miradi 191 ambayo ni asilimia 9.45 na sekta ya Tano kwa kufanya vizuri katika kipindi cha awamu ya sit ani sekta ya Kilimo yenye miradi 180 ambayo ni asilimia 8.91. 


Mwisho.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI