Header Ads Widget

MEZA YA MAGAZETI J5 FEB 26/2025: OFISI YA PAPA YASEMA AFYA YAKE INA AHUENI , VIJANA WENYE ULEMAVU 130 MUFINDI WAFIKIWA NA MRADI WA YAM

div class="separator" style="clear: both;">

 



 MRADI WA YAM WAWAPA MAFUNZO YA KIUCHUMI VIJANA WENYE ULEMAVU 130 MUFINDI 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, MUFINDI 

 HALMASHAURI ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Kwa kushirikiana na mradi wa Youth Angency Mufindi (YAM) imeanza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye Ulemavu 130 kutoka vijiji 16 kata za Ihanu, Mdabulo na Luhunga wilayani Mufindi mkoani Iringa. 

 Meneja wa Mradi wa YAM Zilipa Mgeni amesema Jana kuwa Mafunzo hayo ya Siku 15 yamelenga Kuwasaidia Vijana hao kupata elimu mbalimbali za ujasiriamali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi . 

 Alisema Mafunzo hayo yaliyoanza wiki iliyopita yanaendelea katika ukumbi wa Yatima Kijiji Cha Igoda kata ya Luhunga .

 Alisema mafunzo hayo yatawasaidia Vijana hao Pindi watakapotoka hapo kwende kuanzisha shughuli zao wenyewe . 

 Kwani alisema kupitia mafunzo hayo washiriki watapatiwa elimu ya kutosha ya kukabiliana na kujimudu Kuendesha maisha badala ya kuwa tegemezi. 

 "Wilaya ya Mufindi ni wilaya inayofanya vizuri Katika Kilimo Cha miti hivyo mafunzo haya Kwa Vijana hawa ni moja kati ya mafanikio ya kukabiliana na majanga ya changamoto za kukosa fursa za kiuchumi " alisema 

 Kupitia mafunzo hayo washiriki watapatiwa elimu ya Masomo ya kujitegemea kupitia shughuli watakazochagua wenyewe zikiwemo za kilimo . 

 Alisema Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwajali watanzania wote na Wao kupitia Mradi wa YAM wanaunga mkono jitihada hizo . 

 "Kupitia Mradi wa YAM Vijana hawa Watakuwa mabalozi wazuri kwenye vijiji vyao na wakakuwa msaada mkubwa kwa kufanya kazi badala ya kushinda vijiweni" 


 Huku washiriki wa mafunzo hayo wamepongeza mradi wa YAM Kwa kuwateua kushiriki mafunzo hayo na kuahidi kiyatumia mafunzo hayo kuleta matokeo mazuri kwenye Jamii. Diwani wa kata ya Luhunga Adam Mgovano alisema Mradi wa YAM umekuwa na faida kubwa kwa kata yake na kata shiriki . 

 Kuwa mafunzo Kwa Vijana wenye Ulemavu ni Mafunzo yenye tija kubwa na yatasaidia Vijana hao kuwa mfano mzuri kwa wengine . 

 Mradi wa Youth Angency Mufindi unatekelezwa na Halmashauri ya Mufindi chini ya mradi wa Foxes Community and Wildlife Conservation( FCWC) na YAM kupitia ufadhili wa Finland utakelekelezwa kwenye kata za Luhunga ,Ihanu na Mdabulo ni mradi unaonufaisha vijana na watoto wanaotoka katika familia duni . Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI