Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, leo hii amefunga mafunzo kwa maafisa waandikishaji ngazi ya kata kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 06-07/02/2025 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete. Mafunzo hayo yamekamilika kwa watendaji hao na kuwawezesha kutoa mafunzo kwa waandikishaji wa daftari la kudumu ngazi ya kituo.
Mafunzo kwa waandikishaji wa daftari la kudumu ngazi ya kituo yatafanyika tarehe kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 10-11/02/2025 katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya Lugoba.
0 Comments