Header Ads Widget

KESI YA MAUAJI YA KATIBU CCM KILOLO YAAHIRISHWA HADI MACHI 3

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Kesi ya mauaji ya aliyekuwa Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo Christina Kibiki imeahirishwa hadi machi 3 mwaka huu kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Mbele ya hakimu mkazi mkuu Mahakama ya wilaya ya Iringa Rehema Mayagilo Leo mawakili wa Jamhuri  Radhia Njovu na Cecilia Mrisho uliiiomba mahakama kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na kuendelea na upelelezi ambao umebakiza siku 30 ili ukamilike kisheria.

Upande wa utetezi unaowakilishwa na Barnabas Nyalusi, Gloria Mwandelema, na Neema Chacha kutoka kampuni ya mawakili ya BLS  Attorney &Partner wameiomba Mahakama ya umeiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa wiki moja kwa kuwa imekuwa na ikivuta hisia za watu wengi wanaofika kwaajili ya kusikiliza.



Baada ya kusikiliza pande zote mbili za jamuhuri na utetezi hakimu mkazi mkuu wa mahakama  hiyo aliahirisha kesi hiyo hadi machi 3 mwaka huu kwa kuwa muda wa upelelezi kisheria bado haujaisha. 

Hakimu Mayagilo alisema kuwa upelelezi unatakiwa ukamilike ndani ya siku 90 na lakini hadi leo zimekamilika siku 60 hivyo bado kunamuda wa siku 30 za kukamilisha upelelezi.

 Akijibia suala la ombi la upande wa utetezi juu ya kesi hiyo kurudi baada ya siku saba amesema kuwa washtakiwa ambao makosa yao hayana dhamana wanatakiwa kurudi mahakamani siku zisizozidi kumi na tano hivyo washtakiwa wamepangiwa kurudi mahakamani ndani ya 15 ambayo ni machi 3 mwaka huu.

Watuhumiwa wote wameendelea kusalia kimya bila kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Washitakiwa wamerudishwa rumade hadi machi tatu mwaka huu itakapoletwa kwaajili ya kutajwa tena.

Nje ya mahakama wakili wa upande wa utetezi Gloria Mwandelema akazungumza na waandishi wa habari.


Awali washtakiwa walipelekwa katika mahakama ya wazi ambapo ndugu walijitokeza kama kawaida kusikiliza kesi hiyo na wengine kufika kuwaina ndugu zao hata hivyo baada ya muda mfupi afisaa wa jeshi la polisi alifika mahakamani hapo na kusema kuwa kesi hiyo inaenda kutajwa katika mahakama ya chemba ambapo ndugu wakiendelea kusalia katika mahakama ya wazi.

Hata hivyo ndugu wa upande wa washtakiwa liofika kusikiliza kesi hiyo walionekana kuhamaki baada ya kupigwa picha kabla ya mahakama kuanza huku ndugu wa upande wa marehemu christina Kibiki wakiwa wametulia kusubiri taarifa ya mahakama juu yatarehe nyingine ya  kutajwa kwa kesi hiyo.

MWISHO 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI