Header Ads Widget

JIMBO LA SAME MASHARIKI LILIVOFUNGUKA KIMAENDELEO.



NA WILLIUM PAUL, SAME. 


MKOA wa Kilimanjaro ni mkoa ambao unapatikana Kaskazini kwa Tanzania ukiwa na jumla ya wilaya sita na majimbo ya uchaguzi tisa.


Jimbo la Same mashariki linalopatikana katika wilaya ya Same ni miongoni mwa majimbo ya Ubunge katika mkoa huo linaloongozwa na Mwanamke shupavu na mchapa kazi Anna Kilango Malecela. 



Jografia ya jimbo hilo asilimia kubwa ya wananchi wake wanaishi sehemu ya kilimani ambapo wanajishughulisha kwa kiasi kikubwa na kilimo.


Usilolijua ni asilimia 70 ya zao la Tangawizi inayotumika hapa nchini huzalishwa katika jimbo hilo ambapo huwasaidia wananchi hao kujipatia kipato kwa mtu mmoja mmoja na pia kuliingizia Taifa kipato. 



Miongoni mwa wananchi ambao wamenufaika na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni wananchi wa jimbo la Same mashariki ambapo serikali imewekeza fedha nyingi za miradi ya maendeleo. 


Amina Rashidi ni mkazi wa kata ya Miamba anayejishughulisha na kilimo cha Tangawizi anadai kuwa katika sekta ya kilimo wao kama wakulima hakuna wanachomdai Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ameweza kuwaboreshea mifereji ya umwagiliaji. 



Amina anadai kuwa, hapo awali walikuwa wakilima kilimo kisicho na tija kutokana na maji mengi kupotea njiani kutokana na miundombinu ya mifereji kuwa mibovu lakini kwa sasa wanazalisha mazao kwa tija kubwa na hii ni kitokana na uboreshwaji mkubwa wa miundombinu ya umwagiliaji iliyofanywa na serikali. 


"Shughuli yetu kubwa ambayo tunaitegemea huku kwetu ni kilimo lakini tulikuwa na tatizo la ubovu wa miundombinu ya umwagiliaji hali hii ilikuwa ikituumiza sana na kupelekea kulima na kuvuna mazao kidogo" Anasema Amina. 



Na kuongeza "tangu serikali ilipokarabati miundombinu ya umwagiliaji tumekuwa tukifurahia kilimo kwani tunalima na kuvuna mazao mengi tofauti na kipindi cha nyuma".


Mbali na sekta ya kilimo lakini pia serikali imeweza kuwekeza fedha nyingi katika sekta ya miundombinu ya barabara ambapo hili lilikuwa kero kubwa kwa wananchi hao.



Kutokana na jografia ya Jimbo hilo kuwa ni milimani wananchi walikuwa wakiteseka sana katika usafiri na usafirishaji wa mazao yao kufika masokoni. 


Hatua hii kwa sasa imegeuka kuwa kicheko kwani serikali imeweza kuwekeza fedha nyingi ya kuzikarabati barabara za milimani ambapo kwa sasa wananchi wanauhakika wa kusafiri na kusafirisha mazao yao kipindi chote cha mwaka mzima. 



Rehema Mmbaga mkazi wa Kata ya Vunta anasema kuwa, awali usafiri wa kutokea Hedaru hadi kufika Vunta ulikuwa ni changamoto kwani barabara ilikuwa katika hali mbaya. 


Rehema anadai kuwa, kipindi cha kiangazi walikuwa wakitumia usafiri wa bodaboda lakini kipindi cha mvua walikuwa wakilazimika kutumia miguu ambapo lilikuwa tatizo kubwa hasa wanapokuwa na wagonjwa wanaohitaji kufika katika hospitali ya wilaya ya Same wengi walikuwa wakifia njiani. 


"Wakinamama wajawazito walikuwa wakiteseka sana huku wengine wakilazimika kujifungulia njiani tunaishukuru sana serikali kwa kuona umuhimu wa kutujengea barabara" Amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI