Na Matukio Daima media
Tume huru ya Uchaguzi nchini (INEC) inatarajia kuanza zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha kuanzia Februari 13 hadi 19 mwaka huu.
Aidha jumla ya vituo vya uandikishaji 131 vimeandaliwa kwenye Kata 14 na Mitaa yote 73
Akihitimisha mafunzo ya siku mbili yaliyoanza Februari 10 hadi 11 Februari kwa maofisa waandikishaji ngazi ya Jimbo na Kata, ofisa mwandikishaji Jimbo la Kibaha Mjini Dk Rogers Jacob Shemwelekwa amewapongeza kwa kushiriki kikamilifu Mafunzo hayo yaliyolenga kuwapa ujuzi, weledi na maarifa ili kufanya kazi hiyo ya kitaifa kwa tija
"Ninaamini kuwa kukamilika kwa Mafunzo haya kumetokana na Moyo wenu, usikivu, kujituma na kushiriki kikamilifu katika hatua zote za Mafunzo.Siku zote kazi ni ibada, ukipewa ifanye kwa uaminifu"amesema Dk Shemwelekwa
Kwa mujibu wa INEC uboreshaji utahusisha kuandikisha Wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania waliotimiza miaka 18 na zaidi ambao hawakuwahi kujiandikisha,kuandikisha Wapiga kura ambao watatimiza miaka 18 siku ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 pamoja na uboreshaji wa taarifa za Wapiga kura waliohama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine la Uchaguzi.
Kaulimbiu za zoezi za uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura,2025 inasema _"Kujiandikisha kuwa mpiga Kura ni Msingi wa uchaguzi bora"_
mwisho
0 Comments