Header Ads Widget

ARV HAZIUZWI, ZIPO ZA KUTOSHA -WIZARA YA AFYA


SERIKALI kupitia kwa Wizara ya Afya imebaini uwepo wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vingine 

vya habari zikielezea uhaba wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV), na kwamba sasa watumiaji wanalazimika kununua dawa hizo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa kwa Umma iliyotolewa leo 8 Februari, 2025 na Bi. Roida Andusamile Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya imebainisha kuwa, 

Taarifa hizo ni za upotoshaji na zimeleta hofu miongoni mwa wananchi na kusababisha baadhi ya wagonjwa kuomba kupewa dawa za muda mrefu kwa ajili ya akiba, jambo ambalo si sahihi na linaweza kuathiri utunzaji na matumizi sahihi ya dawa.

"Serikali kupitia Wizara ya Afya, inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI haziuzwi na kwamba zipo za kutosha.

Watumiaji wa dawa hizi, hawana sababu ya kuwa na wasiwasi kuhusu upatikanaji wa dawa hizi. Serikali kupitia Wizara inaendelea kuweka mikakati thabiti na stahiki ili kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida." Imebainisha taarifa kwa Umma.

Aidha, Wizara inatoa rai kwa wananchi kupuuza taarifa hizi na kuendelea kutumia dawa kwa usahihi kama wanavyoelekezwa na wataalam wa afya ili kuzuia usugu wa vimelea vya magonjwa haya dhidi ya dawa."




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI