Header Ads Widget

TANZANIA NA JAPAN KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UCHUMI

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Japan zimeazimia kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji. 


Hayo yamejiri wakati wa mazungumzo kati ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi (Mb.) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Hiyasuki Fuji yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

akimwakilisha Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Hiyasuki Fuji yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam. 

Waziri Chumi ambaye alikutana na Mhe. Fuji kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo amemweleza Mhe. Fuji kuhusu jitihada zilizofanywa na Serikali ya Tanzania ikiwemo maboresho ya mifumo ya kodi na maboresho ya sheria za uwekezaji, kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

 “Licha ya maboresho ya mazingira ya uwekezaji yaliyofanywa nchini, chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzani inatoa fursa hadhimu kwa wawekezaji wa kulifikia soko kubwa zaidi barani Afrika kutokana na nafasi yake ya kijiografia kwa gharama nafuu,” alieleza Naibu Waziri Chumi. 


Vilevile Naibu Waziri Chumi ameleza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Japan katika majukwaa na masuala mbalimbali ya kimataifa yanayolenga kuleta ustawi wa kijamii na kiuchumi ikiwemo masuala ya ulinzi na usalama. Vilevile aliongeza kusema kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za Japan katika kuleta maendeleo barani Afrika kupitia njia mbalimbali ikiwemo shirika la JICA na jukwaa la TICAD. 

Kwa upande wake, Mhe. Hiyasuki Fuji amesisitiza kuwa Japan inaitazama Tanzania kama mshirika muhimu wa kibiashara, hivyo itaendelea kuwekeza zaidi katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi, sambamba na kusaidia juhudi za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji zinazoendelea nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI