Na. Matukio Daima App, Zanzibar.
MABINGWA wa Kombe la Mapinduzi Team ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) inatarajiwa kuwasili Unguja kesho saa 3 kamili asubuhi kwa Ndege mbili Maalum zilizotolewa na Mfanyabiashara Maarufu Abdulsatar.
Mara baada ya kuwasili Kombe hilo litazunguushwa katika Maeneo kadhaa ya Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo baadae Team na Viongozi watapata fursa maalum Ikulu kuhudhuria Mualiko wa Chakula cha mchana uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi (SMZ),Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi alioutoa jana mara baada ya kuwakabidhi kikombe.
Leo Kombe hilo linatembezwa katika viunga vya Pemba na kesho asubuhi msafara huo wa team na Viongozi wake utawasili Unguja.
Shime Wananchi wote tujitokeze kwa wingi kuwapokea Mashujaa wetu.
Aidha, Mratibu Mkuu wa timu hiyo ya Taifa, Hassan Mussa Ibrahim (Has T), amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi katika viunga mbalimbali utakapopita msafara huo wa team ya Taifa kuilaki na kushangilia ushindi huo ambao ni wa Kihistoria.
0 Comments