Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Njombe Mjini ambaye aliyekuwa mgombea uenyekiti serikali za mitaa Mtaa wa Kambarage Emmanuel Kayombo na wenzake Saba wamehama Chama hicho na kutimkia Chama Cha mapinduzi CCM.
Mwaka 2020 Kayombo aligombea udiwani kata ya Njombe Mjini Kupitia Chadema lakini halufanikiwa kushinda Hadi Mwaka 2024 alipogombea uenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kambarage ambako Nako aliangukia Pua dhidi ya Francis Msanga(FM) wa CCM aliyekuwa akitetea kiti hicho kwa awamu nyingine.
Zoezi la kurejea CCM limefanyika katika Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe na kupokelewa na katibu wa Siasa Itikadi uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Njombe Ndugu Josaya Luoga ambaye amewataka kuanza kazi ya kukiimarisha Chama hicho mara moja.
Luoga amesema Uamuzi waliouchukua ni mzuri na wa busara kwani mtaji wa Chama chochote Cha Siasa ni watu na hivyo wapewe Ushirikiano wa Kutosha katika jambo lolote.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama Cha mapinduzi Bwana Emmanuel Kayombo na wenzake amesema kilichowavutia kwenda CCM ni Katiba Imara na yenye misingi ya Kuigwa pamoja na Nidhamu kubwa iliyopo ndani ya CCM.
Aidha Kayombo amesema Chama alichokuwepo Cha Chadema kimekosa Nidhamu na kuweka hadharani mambo ya kuyajadili ndani jambo lililomfanya atimkie CCM kwani hakuna yeyote anayeweza kufanikiwa bila kuwa na Nidhamu.
Kayombo amesema hata katika mkoa wa Njombe Chadema Wamekuwa na mpasuko mkubwa hususani viongozi kwani kila Mmoja anajiona ni mkubwa na hakuna vikao vinavyoweza kuyamaliza matatizo ndani ya Chama.
Naye Diwani wa kata ya Njombe Mjini Alatanga Nyagawa aliyewahi kufanyakazi na Kayombo wakiwa Chadema Amesema CCM kwa sasa imebadilika na haisumbui wananchi jambo linalovutia upinzani kuendelea kujiunga na CCM.
Kwa upande wao baadhi ya wanachama Cha mapinduzi CCM wamesema kitendo Cha wanachadema hao kujiunga na Chama Cha mapinduzi CCM kinawapa nguvu ya kuendelea kulitumikia Taifa na Chama ili kufikisha Maendeleo kwa wananchi.
0 Comments