Header Ads Widget

CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA TLS CHA BURUZWA MAHAKAMANI KWA KUKIUKA HAKI YA KIKATIBA

 


Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS kanda ya Tabora kimeburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kukiuka haki ya kikatiba dhidi ya  ndugu Mohamed Thabiti Nombo wa mkoani Tabora.


Chama hicho kimeburuzwa mahakamani kwa shauri la kesi namba 31308 ya mwaka 2024 dhidi ya Chama hicho cha Wanasheria wa Tanganyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mkoa wa Tabora Mheshimiwa Gabriel Ngaeje ambayo imesomwa kwa mara kwanza siku ya tarehe 7 Januari 2025.



Shauri la kesi hilo limefunguliwa na ndugu Mohamed Nombo ambaye Chama hicho cha Wanasheria kimepeleka malalamiko yake kwa Mheshimiwa Jaji Mfawidhi Kanda ya Tabora kuhusiana na ndugu Nombo kuwa Mawakili waliopo katika Kanda yao ya Tabora kuwa Nombo amekuwa akijihusisha na kazi za uwakili kama kuandaa nyaraka za Mahakama, kuingia mahakamani kuwakilisha wadaiwa kwa kigezo cha kutumia nguvu ya kisheria kinyume na utaratibu wa kisheria.



Shauri hilo kwasasa lina subiri upande wa TLS uweze kujibu tuhuma za malalamiko hayo hicho na limepangwa kutajwa tena mahakamani hapo siku ya tarehe 21 mwezi huu.

Mwishoo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI