Header Ads Widget

WIKI YA PARACHICHI KUANZISHWA MKOA WA NJOMBE

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mkoa wa Njombe unakusudia kuanzisha wiki ya parachichi itakayowakutanisha wadau wote wa zao hilo pamoja na makampuni yanayonunua ili kuliongezea thamani tunda hilo kitaifa na kimataifa na kusaidia kukuza uchumi wa wananchi.


Akifungua mkutano wa Wadau wa Parachichi mkoa wa Njombe kwa niaba ya mkuu wa mkoa,Mkuu wa wilaya Ya Makete Juma Sweda amesema zao hilo la kimkakati linapaswa kuwekewa mkakati mzuri wa kuliboresha ikiwa ni pamoja na kuandaa siku au wiki maalumu ya Parachichi kwa  ngazi ya mkoa.

Baadhi ya wakulima wa Parachichi mkoani Njombe akiwemo Mariam Smalling na Onesmo Mwajombe  wamelalamikia tabia za Madalali wa zao hilo  wanaolangua kwa bei ndogo huku wakiomba muongozo wa serikali.

Hata hivyo wakulima hao pia wamelalamikia changamoto ya miundombinu ya Barabara mashambani vipimo na wadudu kwamba imekuwa kikwazo kikubwa katika sekta ya Kilimo.


Akizungumza kwa niaba ya Wanunuzi wa Parachichi Bwana Hans Byanda amesema wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kutofautiana kwa ushuru kati ya wilaya moja na nyingine huku Magetini kukiwa kikwazo kwa kukalisha mzigo unaooza.

Changamoto za miundombinu ya barabara zimetajwa kuanza kushughulikiwa katika maeneo ya kuelekea mashambani ambapo Mhandisi Costantine Ibengwe Meneja wa Tarura wilaya ya Njombe Kwa niaba ya Tarura Mkoa anakiri kuanza kuchukua hatua.


Msimu wa Mavuno katika tunda la Parachichi unatarajia kuanza mkoani Njombe licha ya baadhi yao kuanza kuchuma huku wito ukitolewa kwa serikali kutoa haraka vibali hivyo wakati bei zikiwa nzuri.

Ofisa Kilimo mkoa wa Njombe Wilson Joel amesema bado mkoa haujafungua msimu wa mavuno ya zao hilo na hivyo wakulima wanapaswa kuvuta subira mpaka matunda yakomae.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI