Na Shemsa Mussa -Matukio daima Blog Kagera
Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati Mhe Dotto Biteko amewataka wazawa wa mkoa wa Kagera wanaoishi nje na ndani ya nchi kutumia fursa ya Ijuka Omuka ili kuendele kuwekeza na kuinua uchumi wa Mkoa huo
Waziri Biteko ametoa wito huo wakati akiongea katika ufunguzi wa tamasha la ijuka omuka katika ukumbi wa KCU uliopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera
Tamasha hili la ijuka omuka limebeba neno la kihaya lenye maana ya kumbuka nyumba ambao limeandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa huo pamoja na wadau wa maendeleo mkoani humo lengo likiwa ni kuwataka wazawa wa Kagera kukumbuka nyumbani na kuwekeza ili kuinua mkoa wa Kagera kiuchumi.
Kwa upande wake Waziri wa mambo ya ndani Inocent Bashungwa alisema wataendelea kushirikiana na mkuu wa mkoa huo ili kuhakikisha wanasukuma mbele maendeleo ya mkoa huo huku akiishukuru Serikali kuendelea kuwekeza Kagera.
Naye Mkuuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema tamasha hili limezaaa matunda mbali mbali ikiwa ni kuanzisha viwanda vipya mkoani humo pamoja na mambo mengi ya kimaendelea
Kwa upande wake mkurugenzi wa kuendeleza kilimo Tanzania Daktari John Kyaruzi alisema kuwa mradi wa uwekezaji wa vizimba mia nne hamsini tayari umepata muwekezaji kutoka Nchini Marekani.
Wakati huohuo mhadhiri wa chuo kikuu Cha sokoine Daktari Philmon Nyinondi akisema tayari taasisi ya tume ya sayansi COSTEC wametenga fedha Kwa ajili ya utafiti wa njia Bora ya uvunaji wa senene.
Tamasha hili la pili la uwekezaji la Mkoa wa Kagera limezinduliwa rasmi leo na litaendelea mpaka Desember 26 mpaka huu.
0 Comments