Faraja Mkuye kutoka dawati la jinsia polisi wilaya ya Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima Kigoma
UKATILI wa kingono umeendelea kuchukua sura mpya mkoani Kigoma ambapo katika miezi miwili Watoto wawili wa kiume wamelawitiwa hadi kusababisha vifo vyao huku mtoto mmoja wa kike akidaiwa kubakwa na baba yake mzazi.
Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashidi ChuaChua ametoa taarifa hiyo katika kongamano la wanafunzi wa vyuo mbalimbali manispaa ya Kigoma ikiwa sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili.
Dk.Chuachua alisema kuwa katika matukio yote matatu ambayo watu wa karibu na familia wanahusishwa tayari jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na uslama vimechukua hatua kuhakikisha waliosababisha madhira hayo wanakamatwa na kuchuliwa hatua za kisheria.
Sambamba na hayo Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa amemuondoa muhudumu mmoja idara ya afya bila kutaja kituo chake wala jina lake akituhumiwa kuandika taarifa potofu ikiwa ni kuharibu Ushahidi wa kesi za kubaka na ulawiti ambazo zimekuwa zikifanyiwa uchunguzi kwa ajili ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa dawati la jinsia la jeshi la polisi wilaya Kigoma, Koplo Faraja Mkuye alisema kuwa kesi za ukatili wa kijinsia hasa ukatili wa kingono zimekuwa na changamoto kubwa kwa wazazi na wadau mbalimbali kujaribu kuharibu Ushahidi au kutotoa ushirikiano ili kuhakikisha mashauri ya kesi hizo Kwenda mahakamani yanakwama.
Akizungumza katika kongamano Afisa elimu kwa mlipa kodi mkoa Kigoma, Makilo Seuta Lukulunge alisema kuwa mamlaka ya mapato (TRA) mkoa Kigoma inaungana na wadau katika kupinga vitebdo vya ukatili kwa jamii kwani watu hao ni walipa kodi hivyo wanapopatwa na masuala ya ukatili na kushindwa kulipa kodi jambo hilo linaikosesha serikali mapato.









0 Comments