MKUU WA MKOA WA MBEYA JUMA HOMERA
Na Thobias Mwanakatwe, MBEYA
OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na kampuni ya Mc Edwin Luvanda Branding and Entateiment imeandaa tamasha la vyuo vikuu na vyuo vya kati ambalo litawashirikisha wanavyuo zaidi ya 2000 wa vyuo vilivyopo mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa kampuni ya MC Edwin Luvanda,akizungumza leo (Disemba 5, 2024) na waandishi wa habari, amesema tamasha hilo ambalo litakuwa na kauli mbiu isemayo ‘Kuelekea Miaka 30 ya Beijing Chagua Kutokomeza Ukatili litafanyika katika Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mbeya Disemba 9. Mwaka huu ambayo itakuwa ni siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika.
Luvanda amesema lengo kuu la tamasha hilo ni kutangaza na kuviweka pamoja vyuo vilivyopo Mkoa wa Mbeya pamoja na kutangaza fursa za utalii zilizopo Mkoa wa Mbeya ili kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi waweze kuvitembelea.
Amesema wakati wa tamasha hilo michezo itakayofanyika ni mpira wa miguu kwa wanawake na wanaume,mpira wa pete na kuvuta kamba.
Luvanda ameongeza kuwa shughuli nyingine zitakazofanyika ni uchangiaji wa damu kwa hiari na huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa hiari.
Mkurugenzi huyo amewaomba wanavyuo na wananchi wa Mkoa wa Mbeya kwa ujumla kujitojkeza kushiriki tamasha hilo ambalo ni la muhimu sana katika kuutangaza Mkoa wa Mbeya.
Kampuni ya Mc Edwin Luvanda Branding and Entateiment imekuwa ikiandaa shughuli mbalimbali kwa mikoa ya nyanda za juu ambapo mwezi Oktoba 2024 iliandaa Usiku wa Dhahabu hafla ambayo iliwashirikisha wachimbaji madini kutoka mikoa ya Mbeya na Songwe.
0 Comments