Watalii wa ndani na wa nje zaidi ya 300 wanatarajia kutembea katika tamasha la matembezi ya msituni katika hifadhi ya mazingira asilia ya msitu wa Magamba ili kujionea mazingira ya msitu wa asili iliyotunzwa na Wakala wa Misitu TFS.
Hayo yamesemwa na Mhifadhi Mwandamizi Misitu wa Wakala wa misitu TFS wilaya ya Lushoto Hassan Sengerere wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika vilele vya milima ya Usambara huko Kigulu Hakwewa Lushoto mkoani Tanga.
Amesema Matembezi hayo msituni ni sehemu ya kuhamasisha Utalii hivyo watembeaji wataweza kuona mnyama wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbega mwenye Rangi Nyeusi na nyeupe na Mandhari ya kuvutia katika msitu wa Magamba.
''Tuliamua watu watembee badala ya kukimbia katika matembezi hayo maalufu kwa Nina 'Magamba forest Walkathon & Adventure season 2 kuanzia 4-7 Desemba 2024'' na kuhusisha wadau na wananchi wote kwa ujumla' kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano asubuhi kwa lengo la kuboresha na kuhamasisha utalii" alisema Sengerere.
''Ni muda muhafaka wa watu kuja kujionea vivutio mbalimbali vilivyomo katika misitu ya hifadhi asilia wa Magamba ambako kuna pia Maporomoko ya maji yapo, mimea ambayo ipo katika misitu hiyo tu hakuna katika misitu mingine duniani'' alisema.
Alisema Watalii hao watatembea katika maeneo mbalimbali ya milima hiyo hasa katika msitu wa Magamba ambapo watajionea wadudu vivutio ambao ni pamoja na vipepeo, kinyonga kivutio wenye pembe tatu na kinyonga mwenye pembe mbili.
Aliongeza kuwa pia watalii hao wakati wanatembea msituni humo watajionea vivutio vya wanyama kama Tumbili na mbega wenye rangi nyeupe na nyeusi ikiwa kuhamasisha utalii katika msitu huo wa Magamba huko wilayani Lushoto mkoani Tanga.
Hifadhi ya msitu wa Magamba imefunikwa ni miti mikubwa ya asilia yenye muonekano na Mandhari nzuri Kwa watalii sambamba na bwawa lenye Bata wakuvutia Watalii.
''Mwaka jana 2023 watalii zaidi ya 4000 kwa wastani wa watalii wa ndani na nje 350 kwa mwezi walifika kutembea na kujionea vivutio mbalimbali katika misitu yetu ya Magamba wilayani Lushoto mkoani Tanga'' alisema
Kwa upande wake Mratibu wa tamasha la matembezi msituni katika msitu wa Magamba Nelson Machibya ameeleza namna tamasha Hilo litavyokuwa na kiasi Cha kilomita ambazo Washiriki watatembea kuwa ni pamoja na matembezi ya kilomita 5, kilomita 10, 20 na matembezi ya kilomita 40 kwa baiskeli.
''Watalii hao watatembea msituni humo huku wanaangalia vivutio mbalimbali vilivyomo katika misitu hiyo kulingana na kilomita zao watakazoamua kutembea'' alisema Machibya.
0 Comments