Header Ads Widget

WABUNGE WATATU MAJERUHI AJALI YA BASI LA SHABBY WAHAMISHIWA MOI

 


Wabunge watatu majeruhi wa ajali ya basi la Kampuni ya Shabiby waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, wamehamishiwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili-MOI kwa matibabu zaidi.


Desemba 6 mwaka huu, wabunge 16, maofisa wawili wa Bunge na dereva wa basi hilo walijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Mbande, wilayani Kongwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kwenda kwenye michezo ya Afrika Mashariki, Mombasa nchini Kenya, kugongana na lori lililokuwa likitoa Morogoro kuelekea Dodoma.

 Meneja Mawasiliano MOI, Patrick Mvungi amesema wamepokea wabunge watatu kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mvungi amewataja wabunge hao kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar, Mwanakhamis Kassim Said, Mwakilishi wa Jimbo la Amani Zanzibar, Abdul Yusufu Maalim pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Furaha Matondo.

Vilevile wabunge wengine 13 waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa baada ya kupata ajali hiyo wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI