Header Ads Widget

VIJANA WANAOTOA HUDUMA ZA UKARIM WATAKIWA KUWA WAAMINIFU



NA HAMIDA RAMADHAN, MATUKIO DAIMA APP DODOMA


MKUU wa Wilaya ya Bahi  Rebecca Sanga amewataka Vijana wote wanaosomea Sekta Ukarimu na watoa huduma ya ukarimu kwa ujumla Mkoani Dodoma kuhakikisha kuwa wanakuwa waaminifu,Wasafi na Wachangamfu nyakati zote wawapo katika majukumu yao kwani uaminifu siku zote unalipa.

 Rebecca ameyasema hayo Jijini Dodoma katika Kongamano la Wadau wa Sekta ya Ukarimu na Utalii lililofanyika katika chuo cha Ufundi Stadi Veta Dodoma. 


Amesema kuwa sekta ya Ukarimu ni nguzo muhimu sana katika Mkoa,lakini sekta hii si kwamba inachangia pato la mkoa tu bali linatoa ajira kwa vijana wetu.

Aidha Sanga amesema Serikali ya Mkoa wa Dodoma imeweka usalama wa kutosha hivyo watu wanaweza kutanua biashara kwa kkufanya muda wote kwasababu usalama upo na anatarajia kuona Dodoma ikishamiri.


"Kwahiyo niwasihi sana ndugu zangu Tasnia yetu inahitaji ukarimu,Usafi na Uchangamfu kwa tunaowahudumia,tuna hitajika kuwa wakarimu kweli kweli kwani uaminifu na ukarimu unalipa".


Naye Ramadhani Ali Mataka ambaye ni Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Kati amesema lengo na madhumuni ya kukutana na wadau wa sekta ya Ukarimu na Utalii mkoa wa Dodoma ni kuona namna gani bora ya kutatua changamoto zinazoikabiki sekta hii kwani Dodoma ni mji Mkuu na watu wengi wanaingia kila siku,hivyo ni vema wageni watakapoingia wakakutana na Ukarimu wa hali ya juu,kwani sekta hii imekuwa ikilalamikiwa sana.

Wakati akitoa taarifa ya Chuo cha Veta Dodoma, Mkuu wa chuo hicho Bwana Deodatus Orotha amesema kuwa  chuo kinaendelea kutoa mafunzo yanayokidhi viwango ili kuendana na soko la Dunia hasa katika Sekta hii ya Ukarimu


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Veta Tanzania CPA Anthony Kasore amesema kuwa kwasasa wana vyuo 80 vinavyotoa mafunzo ya Ufundi katika Mikoa yote Nchini, na vipo vyuo 65 vinavyoendelea kujengwa katika mikoa hiyo vinavyojumuisha wilaya 64 lakini matarajio ni kuwa ifikapo mwaka 2025 ni Veta kuwa na jumla ya vyuo 145, ili kuendana namono ya Mhe Raisi ya kuwa kila Mtanzania kuwa na ujuzi kutoka katika vyuo vya ufundi Stadi hapa Nchini.


"Sasa hivi tuna vyuo 80 vinavyotoa mafunzo ya ufundi katika mikoa yote na katika mikoa hiyo ujenzi unaendelea wa vyuo 65 vinavyojumuisha wilaya 64. Na matumaini yetu ni kwamba ifikapo  mwaka 2025 Veta tutakuwa na jumla ya vyuo 145 ambavyo vitakuwa ndani ya Mikoa yote na Wilaya zote Nchini".


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI