Header Ads Widget

TWENZETU KILELENI AWAMU YA NNE KUONGOZWA NA ZAIDI YA MABALOZI 10


Na Esther Machangu, Moshi Kilimanjaro

Katika kuelekea kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika, kundi la mabalozi zaidi ya 10, wanatarajiwa kuongoza msafara wa wapanda mlima zaidi ya 235 wakiwemo wanajeshi wa Jeshi la ulinzi Tanzania (JWTZ), wadau wa tasisi binafsi na serikali pamoja na watu binafsi.

Wakizungumza leo Mjini moshi katika hotel ya Springland mabalozi hao wamesema zoezi Hilo la kupanda mlima Kilimanjaro katika sharehe za uhuru ni moja ya kuongeza chachu  ya watalii kutoka katika nchi wanazozisimamia.


Hata hivyo mabalozi hao akiwemo Balozi Simon Sirro wa Zambia, Balozi wa Tanzania nchini Brazil Adelardus Lubango, Balozi wa Tanzania nchini Burundi Gelasius Byakanwa wamepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya uwongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kujudi za kuutangaza Utalii wa Tanzania.

Kwa upande wake wa Kamishna msaidizi wa uhifadhi anayeshughulikia Sheria Ulinzi na Mkakati wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ignas Gala, amesema Kampuni za utalii zilizopewa nafasi ya kuwafikisha wageni katika kilele cha mlima Kilimanjaro ikiwemo ZARA TOURS,AFRICAN SENIC,AFRICAN ZOOM SAFARI, pamoja na hifadhi hiyo ya TANAPA wamejipanga kuhakikisha wageni hao wanafika katika kilele cha Kilimanjaro.


Naye Bernard Sahini mwakilishi kutoka Kampuni ya Zara Tours ambayo inawapandisha wageni hao kupitia njia kuu ya marangu amesema hii ni Mara ya 16 kushiriki katika zoezi Hilo ambapo hapo awali walikuwa wakifanya na Jeshi la ulinzi la Tanzania

Stephan William ni mwenyekiti wa bodi wa shirika la APDN linaloshughulikia watu wenye ulimavu amesema hii itakiwa mara ya kwanza kwa watu wenye ulemavu kushiriki zoezi hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI