Header Ads Widget

TANROADS PWANI KUTEKELEZA MIRADI YA BARABARA KWA MWAKA 2024/2025

UTEKELEZAJI wa miradi ya miradi ya matengenezo ya barabara za mkoa na barabara kuu Mkoani Pwani utatumia kiasi cha shilingi bilioni 29.5 kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage wakati wa kikao cha bodi ya barabara cha Mkoa.

Mwambage amesema kuwa fedha hizo zinahusisha miradi ya maendeleo na matengenezo kwa kipindi hicho.

"Miradi ya maendeleo ni 38 yenye thamani ya shilingi bilioni 18.9 huku ya matengenezo ikiwa ni sita yenye thamani ya shilingi bilioni 10,"amesema Mwambage.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa kutokana na changamoto ya fedha ambapo nchi imefanya uchaguzi hivyo kutumia gharama kubwa miradi ifanyike kutokana na vipaumbele.

Kwa upande wake Petro Magoti amesema kuwa baadhi ya wakandarasi uwezo wao ni mdogo na wanasababisha baadhi ya miradi kuchelewa hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI