Header Ads Widget

SERIKALI KUENDELEA KUIWEZESHA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA NCHINI.

 


Na,Jusline Marco;Arusha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Philip Mpango amesema serikali itaendelea kuiwezesha Takukuru upande wa rasilimali fadha na watu ili iweze kutekeleza wajibu wake wa kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa katika Taifa.

Akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Takukuru,Dkt.Mpango amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiendeleza mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwekeza katika ujenzi wa taasisi imara ikiwemo haki jinai kuoambana na makosa ya jinai pamoja na rushwa.


Dkt.Mpango ameongeza kwa kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuhakikisha ofisi zote za Takukuru zinaunganishwa na mifumo ya Tehama ili iqeze kusomana na mifumo ya taasisi nyingine hususani migumo ya Haki jinai.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bwn.Chrispin Chalamila katika mkutano huo amesema zaidi ya bilioni 18 zimeweza kuokololewa kwa kipindi cha miezi 12 kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi pamoja na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema mkutano huo ni maalumu kwa ajili ya kutatjomini utendejikazi wa taasisi hiyo kwa madhumuni ya kuimarisha na kuboresha utendeji kazi ili kuzidi kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa hivyo kupitia mkutano huo watabainisha mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha mwaka mmoja wa utendajikazi na changamoto walizokabiliana nazo.

Mhe.Deus Sangu Naibu Waziri,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Itawala Bora amesema wizara hiyo itaendelea kisimamia Takukuru kwa mujibu wa sheria kuhakikisha vita dhidi ya rushwa ni mapambano ambayoyanapaswa kitekelezwa kwa nguvu zote 


Kwa upamde wake Waziri wa nchi ofisi ya Rais Kazi maalum na mwenyekiti wa wanachama wabunge wanaopambana na Rushwa Afrika Tawi la Tanzania, George Mkuchika katika mkutano huo ameitaka Takukuru kutobweteka pamoja na imani kubwa iliyopo kwa wananchi, bado wanayo kazi kubwa ya kufanya ili kuweza kudhitibi na kuzuia vitendo vya rushwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI