Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya imeahirisha kusikiliza maombi ya mwanaharakati Mdude Nyagali Mpaluka kufikishwa mahakamani au kuachiwa kwa dhamana juu ya madai anayotuhumiwa ya kisambaza taarifa za uongo mitandaoni.
Mahakama kuu kupitia jaji Victoria Nongwa, imeahirisha shauri hilo la maombi baada ya mawakili wa upande wa wajibu maombi (Serikali) kupitia mawakili Lodgard Eliaman na mwenzake Dominic Mushi wameiomba mahakama kuwapa muda ili kuwasilisha hoja zao za viapo kinzani juu ya madai ya waleta maombi kutaka Mdude Nyagali afikishwe mahakamani au kupewa dhamana.
Kufuatia maombi hayo ya Jamuhuri, jaji Victoria Nongwa wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya ameahirisha shauri hilo hadi Desemba 06, 2024 kwa ajili ya Jamuhuri kutoa hoja zao.
Akizungumza baada ya mahakama kuahirishwa wakili Philip Mwakilima anayemwakilisha Mdude Nyagali pamoja na wakili Boniface Mwabukusi, amesema wanasubiri tarehe tajwa ili kusikiliza hoja za wajibu maombi ambapo maombi yao ni kuona mteja wao (Mdude Nyagali) anafikishwa mahakamani kwa madai kuwa ameshikiliwa na Polisi nje ya muda unaoelezwa na sheria.
0 Comments