Header Ads Widget

RC NJOMBE AKASIRISHWA NA MATUKIO YA MAUAJI NA UKATILI KATIKA JAMII.

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama mkoa wa Njombe  ambaye ni mkuu wa Mkoa Antony Mtaka amekasirishwa na matukio ya kikatili yanayofanywa na baadhi ya watu dhidi ya watu wengine na kwamba vitendo hivyo havivumiliki.

Mtaka ametoa kauli hiyo katika kikao maalum alichoitisha ili kujadili hali ya ulinzi na usalama katika mkoa hususani ukatili unaoendelea katika jamii na kwamba kila mmoja anapaswa kueleza nini kifanyike ili kupunguza matukio hayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema katika kipindi cha mwaka 2024 Kumeripotiwa jumla ya matukio 59 ya mauaji huku zaidi ya 100 ni ya Ubakaji.

Aidha Kamanda Banga amesema pia kumeripotiwa kwa matukio ya ulawiti vitendo vinavyofanywa ndani ya Familia huku Mauaji mengi katika wilaya ya Ludewa yakitajwa kutokana na Imani za kishirikina.

Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe matukio mengi ya mauaji yametajwa kusababishwa na migogoro ya ardhi huku wilaya ya Wanging'ombe na Makete sababu zikichanganyika zikiwemo za Wivu wa mapenzi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Jolam Hongoli,Asante Mgeni na Mabula Kidai wamesema wazazi wanapaswa kuanza kuwachunguza watoto wao tangu wakiwa wadogo wa miaka miwili na kuwasimamia katika malezi huku tamaa ya utajiri kwa baadhi ya vijana bila kufanya kazi halali husababisha matukio hayo.

Wanasema Wazazi wengi wamekuwa wakiachiana majukumu ya malezi katika familia na vijana wa kiume kupenda kulelewa badala ya kuchukua jukumu la kulea familia yake.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI