Na,Jusline Marco;Arusha
Jumla ya wananchi 97 waliokubali kuhama kwa hiari kutoka ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Kwenda Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Tanga, wametoa wito kwa wananchi wenzao waliobaki ndani ya hifadhi kujiandikisha ili wapate uhuru na fursa ya kuboresha maisha yao nje ya Hifadhi na kuepuka hatari ya kuishi na wanyama wakali katika eneo moja.
Wakati kundi la 21 la awamu ya pili lenye kaya 23, watu 97 na mifugo 196 likihama kwa hiari ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Kijiji cha Msomera na maeneo Mengine waliyochagua wenyewe,kundi hilo kupitia wawakilishi wao limewataka wananchi wenzao waliobaki ndani ya hifadhi kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kuboresha maisha yao.
Wakizungumza leo Desemba 19 wawakilishi hao wamewataka wananchi wenzao kufanya hivyo ili kupata uhuru na fursa ya kuboresha maisha yao nje ya Hifadhi kusudi kuweza kuepuka hatari ya kuishi na wanyama wakali katika eneo moja ambapo jumla ya wananchi 97 wamekubali kuhama kwa hiari kutoka ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Kwenda Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Tanga.
Mmoja wa wananchi hao waliohama leo Bw.Daudi Melubo kutoka kijiji cha Kayapus amesema yeye na familia yake waliamua kufanya maamuzi ya kuhama ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa kutokuwa na uhuru wa kujiendeleza kiuchumi kutokana na sheria za uhifadhi huku Bi. Naishiye Sembeta akieleza kuwa wanawake wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta kuni porini huku wakihatarisha maisha yao, ila kwa sasa kuhamia Msomera wanatumaini maisha yao yatabadilika na kuwa bora zaidi.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo, Meneja wa mradi Afisa uhifadhi Mkuu Flora Asey amesema kuwa hadi kufikia leo tarehe 19 jumla ya kaya 1,678 zenye watu 10,073 na mifugo 40,593 zimekwisha hama ndani ya Hifadhi kuelekea Msomera na wengine kwenye maeneo waliyoyachagua wenyewe.
Amesisitiza kuwa kwa sasa utaratibu uliopo ni kuhakikisha kuwa zoezi la uandikishaji, tathmini ya maendelezo na uhamishaji vinaenda sambamba ili kuhakikisha kila mwananchi anapojiandikisha anatumia muda mfupi kuhama ndani ya hifadhi kwenda eneo alilochagua
Zoezi la kuhama kwa hiari ndani ya hifadhi ya Ngorongoro linaendelea ikiwa ni lengo la Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kuwa wananchi hao wanapata fursa ya kuishi katika maeneo salama yenye huduma zote muhimu za kijamii kwa ajili ya maendelea ya wananchi hao.
0 Comments