Header Ads Widget

KIKAO CHA RCC MKOANI ARUSHA KIMEWEKA MIKAKATI YA KUWAONDOA OMBAOMBA HUSUSANI WALIO KATIKA MATAA YA BARABARANI.

Na,Jusline Marco;Arusha

Suala la ombaomba ndani ya mkoa wa Arusha katika maeneo mbalimbali limechukuwa sura mpya baada ya wajumbe katika kikao cha Ushauri cha Mkoa kuweka mikakati ya kuwafuatilia ili kuweza kubaini wanakotoka.

Wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wamesema jambo hilo la walemavu kuomba misaada katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye taa za barabarani ni jambo la muda mrefu ambapo wamewaomba wenyeviti wa mitaa kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini.

Wajumbe hao wamesema kuwa wenyeviti wa serikali za mitaa wana wajibu mkubwa wa kubainisha walemavu hao kutokana na kuwafahamu wakazi wao hivyo ni rahisi kwa wao kuwatambua na kuwabainisha kwani wengi wao ni wageni kutoka mikoa ya jirani.

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Misaile Mussa amesema maeneo ambayo walemavu hao huyatumia siyo salama kwao hivyo kupitia timu ya wataalam wa Mkoa itafuatilia kwa ukaribu suala hilo ambapo ameuelekeza uongozi wa wilaya za mkoa wa Arusha kushughulikia suala hilo kwa kutosababisha ukatilj na kutweza utu wao.

Amesema kwa sasa halmashauri ya jiji la Arusha lina zaidi ya bilioni 6 kwaajili ya kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu ambapo amewataka walemavu hao badala ya kukaa barabarani kuomba misaada na kuhatarisha maisha yao,waombe mikopo hiyo ili waweze kufanya biashara zitakazowaingia kipato.

"Wakishafanya hivyo ndiyo tutabainisha nani yupo barabarani na nani anafanya shughuli halali kupitia mikopo ambayo inayolewa na halmashauri."Alisema Katibu Tawala Mkoa wa Aruaha Missaile Mussa

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda,katika kikao hicho amesema suala hilo limewekewa mkakati kwa maafisa ustawi wa jamii na maafisa maendeleo ya jamii kuhakikisha wanatumia mbinu zao kuwafuatilia walemavu hao ili kujua uhalisia wao.

Ameongeza kuwa kikao hicho pia kimeazimia kila wilaya kutenga maeneo ambayo yatatumika katika masuala ya uwekezaji na utalii ikiwa ni sambamba na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kulingana na maelekezo  yaliyotolewa ya kuwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

Naye Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Danielson Palangyo amewapongeza wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ua Mkoa RCC kwa kutoka na maazimio ambayo yatasaidia katika uletaji wa maendeleo ya jiji la Arusha na uongezaji wa mapato kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Arusha.

Mhe.Palangyo amesema suala la upandishaji hadhi maeneo na kufuta baadhi ya maeneo kutasaidia ukuaji wa maendeleo kwenye maeneo ambayo yamepandishwa hadhi hivyo kuongeza mapato kwa halmashauri na mkoa kwa ujumla.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI