Header Ads Widget

POLISI -NONDO AMECHUKULIWA NA LAND CRUSIER NYEUPE TUNAFUATILIA ..

Huku chama Cha ACT-Wazalendo kikisema mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Abdul Nondo ametekwa leo asubuhi na watu Wasiojulikana na kudondosha pingu wakati wa purukushani za kumkamata , Jeshi la Polisi limesema amechukuliwa na Land Crusier nyeupe na wanafuatilia.

Nondo anadaiwa kukutwa na kadhia hiyo leo Jumapili Desemba mosi, 2024 muda mfupi baada ya kushuka katika basi kituo cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Kigoma alikokuwa akishiriki shughuli za chama hasa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Novemba 27, 2024.

Msemaji wa Polisi, David Misime kupitia taarifa kwa umma amesema: “Jeshi la Polisi lingependa kujulisha kuwa, Disemba 1,  2024 majira ya saa 11.00 alfajiri katika eneo la stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es Salaam kuna mtu mmoja mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili wa namba T 249 CMV aina ya Land Cruiser rangi nyeupe.

“Ilielezwa na mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa ni vya Abdul Omary Nondo.”

Misime amesema ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza baada ya kupokewa kwa taarifa hiyo Polisi, sambamba na kufungua jalada.

TAARIFA YA ACT WAZALENDO 

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Ndugu Abdul Nondo ametekwa asubuhi hii na watu wasiojulikana akitokea Mkoani Kigoma alikokuwa sehemu ya viongozi wa Kitaifa walioongoza kampeni kwenye Mikoa ya Magharibi mwa Tanzania.

Mashuhuda wa tukio wanasema kuwa kulikuwa na purukushani katika utekaji wa Nondo iliyosababisha begi lake ndogo kudondoka. Katibu Mwenezi Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Monalisa Ndala na Afisa wa Harakati na Matukio Taifa Wiston Mogha waliofika mapema kituoni hapo walitambua haraka kuwa aliyetekwa ni Nondo kwa sababu walizitambua nguo zake kwenye begi lililodondoka na note book yake.

Chama kinaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tukio hili na kitatoa taarifa zaidi kwa umma.

Katika hatua ya sasa tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Wambura kufuatilia mara moja na kuhakikisha Ndugu Abdul Nondo anaachiwa huru mara moja.  Anandika Ado Shaibu Katibu mkuu WA ACT wazalendo

Imetolewa na Mbarala Maharagande, Naibu Katibu wa Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi,

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI