Mchungaji, John Chida wa Kanisa la Heri Huruma aliyekuwa akiishi kitongoji cha Isakalilo C, kata ya Isakalilo, Wilaya ya Iringa, alifariki Dunia, Oktoba 2024 akiwa nyumbani kwake, huku akiwa hadi sasa, hajazikwa kutokana na baadhi ya waumini wake wakiaamini hakuwa amekufa, bali amelala na atarudi siku moja kama alivyoahidi.
KITANDA ALICHOKUWA AMELAZWA MCHUNGAJI JOHN CHIDA BAADA YA KUFARIKI DUNIA
Muumini mmoja wa kike, mama aliyeamini maneno ya Mchungaji, alihangaika kila siku tangu Oktoba. Alikuwa akisafisha mwili wa Mchungaji, kumbadilisha nguo, kufunika mashuka, na hata kuweka net ya mbu kwa imani kwamba atarudi hai.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa eneo hilo alipewa taarifa kuhusu hali hiyo na alipochukua hatua ya kuvunja mlango, walikuta Mchungaji ameshafariki dunia kwa muda mrefu. Baadhi ya waumini walidai kwamba alikuwa amelala tu, na hawakuamini kwamba alikuwa amefariki.
Polisi wamechukua mwili wa marehemu na kuupeleka mochwari kwa uchunguzi zaidi, huku mama huyo muumini akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwa mahojiano na hatua zaidi.
Hongera kwa Mwenyekiti wa Isakalilo kwa kuchukua hatua stahiki, na shukrani kwa wasamaria wema walioripoti suala hili kwa wakati ili kuhakikisha ukweli unafahamika.
Mchungaji John Chida wa Kanisa la Heri Huruma, lililopo katika Kitongoji cha Isakalilo C, kijiji cha Isakalilo, Kata ya Kalenga Wilaya ya lringa amedaiwa kuwa amefariki tangu mwanzoni mwa Oktoba 2024 na kutokuzikwa mpaka leo (Desemba 4, 2024) kwa madai aliacha maagizo yakuwa atafufuka.
Majirani wamesema kuwa tangia aanze kuugua mchungaji huyo, alikataa kwenda hospitalini ama kupata matibabu ya aina yoyote na mara ya mwisho kumuona ni mwishoni mwa mwezi wa 9 na tokea kipindi hicho hakutoka tena nje ya nyumba yake huku na wao wakizuiwa kuingia ndani kwake na muumini aliyekuwa akiishi na mchungaji huyo ili kumuona kwa kwa kile kilicho daiwa kuwa haitaji usumbufu.
Wamesema, kwa kipindi chote hicho hawakujua kama mchungaji huyo amekufa na amefungiwa ndani na mama huyo, kutokana na namna alivyokuwa akiendelea na maisha yake kama kawaida.
Aidha, wanaichi hao wameongeza kuwa, baada ya kupata taarifa za kifo cha mchungaji huyo, na kuviita vyombo vya usalama ili kuuchukua mwili wa mchungaji huyo, mwanamke huyo aliwazuia kuuchukua kwa madai kuwa zimebakia siku tatu pekee ili Mchungaji wake awezee kufufuka hivyo wanaharibu utaratibu wa Mungu.
Amosi Msole ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Isakalilo C, ameelezea namna alivyomfahamu mchungaji huyo, na kusema kuwa baada ya kutomuuna kwa muda mrefu aliamua kwenda nyumbani kwake na kwa zaidi ya mara tatu alizuiwa kuingia ndani na mama huyo, na kuambiwa kuwa amepumzika, jambo ambalo lilimpa mashaka siku ya jana na kuamua kutumia nguvu kuingia ndani, na ndipo alipogundua mchungaji huyo alifariki muda mrefu na mwili wake ulikuwa tayari umeharibika vibaya.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Isakalilo Deo Msemwa, amesema, mwili wa mchungaji huyo umekaa ndani kwa zaidi ya takribani siku 45 kutokana kuwaaminisha waamuni wake kuwa yeye hata kufa bali atalala na muda ukifika atafufuka.
Amesema kupitia maagizo hayo aliyoyaacha yamesababisha mwanamke aliyekuwa akiishi naye kuficha taarifa za kifo chake na kuendelea kusafisha mwili pamoja na kubadilisha nguo kila siku licha mwili mtumishi huyo kuendelea kuharibika.
0 Comments