Header Ads Widget

TUKIO LA UTEKAJI WAKILI SI LA KWELI -POLISI

 


Baada ya kusambaa kwa taarifa juu ya watu wanaodhamiwa ni Wasiojulikana kumkimbiza kwa kutaka kumteka wakili Alphonce Lusako , Jeshi la Polisi limetoa   ufafanuzi ili isiendelee kuleta taharuki ambayo siyo ya lazima.

Ni kweli Askari Polisi walifika eneo hilo kumkamata mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mweta, ambaye awali alikamatwa na baada ya kudhaminiwa ambapo mtuhumiwa aliruka dhamana kwa muda mrefu.

Leo Desemba 5,2024, Mlalamikaji alitoa taarifa Polisi kuwa amemuona mtuhumiwa huyo, ikabidi askari wawahi haraka kumkamata,

Tunaendelea na uchunguzi kubaini ni nini kilichomfanya anayetajwa kwa jina la Alphonce Lusako kukimbia kisha kujirekodi video voice na kuirusha kwenye mitandao wakati siyo yeye aliyekuwa anatafutwa na Askari waliofika pale waljitambulisha kwake na kumweleza wamefika pale kwa nia ya kumtafuta Emmanuel Mweta.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI