Header Ads Widget

MASWALI MAZITO YA ASKOFU MWAMAKULA JUU YA KUTEKWA KWA NONDO!

 


Ndugu Watanzania!

Mapema asubuhi ya leo, tuliutaarifu umma juu ya taarifa za kutekwa na watu wasiojulikana kijana mmoja ambapo mashuhuda walisema ni  Mwenyekiti wa ACT Wazalendo bila kuainisha ngazi na pasipo kutaja jina.


Baadaye, ACT Wazalendo kiliuthibitishia umma kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo alitekwa akiwa katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi. 

Katika kufuatilia tukio hili tunabaki na maswali. 


Kutekwa kwa kijana Mwenekibalo Abdul Nondo  inaonekana ni tukio lililoratibiwa vizuri na watu waliokuwa Kigoma, Tabora, ndani ya basi na katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli. Askofu anaufikirisha ubongo wake na kucheua haya:


1. Taarifa za mashuhuda zilieleza kuna kijana mmoja aliyepiga picha tukio pamoja na gari lililomteka Nondo. Taarifa hizo zilieleza zaidi kuwa kijana huyo alichukuliwa na Polisi akiwa na picha zake. Swali ni kama ACT Wazalendo kitajua taarifa za kijana huyo na kama kitapata taarifa ya kuonana naye.


2. Je, kijana aliyepiga picha alikuwa pamoja na Nondo, alikuwa sehemu ya watekaji ambaye alitelekejwa kama mama wa Kiyahudi ambaye alitelekezwa Kampala katika zoezi la Operation Thunderbolt (90 Minutes at Entebbe) mwishoni mwa miaka ya 1970s au kijana huyo alikuwa ni mpita njia tu?


3. Taarifa za ndani zaidi zinaeleza kuwa CCTV camera (kamera za kikachero) zilizopo Kituo cha Magufuli zilipotazamwa, zilionyesha kuwa wakati wa tukio zilikuwa zimeelekezwa upande mwingine tofauti na upande aliotekwa Nondo.


4. Hoja namba 3 inatufikirisha zaidi. Iweje hizo CCTV camera pia zielekezwe sehemu nyingine wakati wa tukio? Je, watekaji hao walikuwa na 'mchongo' au 'dili' na mamlaka zinazoendesha CCTV camera Kituo cha Mabasi cha Magufuli?


5. Taarifa zetu za awali zilisema kabisa kuwa ilijulikana wazi kuwa huyo kijana alikuwa ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo na hata Polisi walipofika walielezwa hivyo na walijua kufuatia vitu vilivyoachwa pale ikiwemo begi, noti book, nk ambavyo ndivyo vilifanya mashuhuda wa tukio waanze kuwatafuta ACT Wazalendo


6. Uongozi wa ACT Wazalendo unaonesha ya kuwa ulipata taarifa kutoka kwa mashuhuda na sio Jeshi la Polisi.


7. Hoja namba 5 na 6 inatufanya tuhoji hekima ya utendaji wa Jeshi la Polisi katika masuala ya aina hiyo kuhusu usalama wa raia. Je, Jeshi la Polisi haliwajibiki kupiga simu kwa ndugu au hata mwajiri kuwajulisha habari za mtu ambaye taarifa zake wanazo?


8. Je, Jeshi la Polisi hawawezi kupata namba za viongozi wa ACT Wazalendo?


Kwa vyovyote vile taarifa juu ya kijana aliyepiga picha tukio ambaye alichukuliwa na Jeshi la Polisi baada ya tukio na taarifa juu ya CCTV camera ni taarifa muhimu kuhusiana na tukio la kutekwa kwa Mwenekibalo Abdul Nondo!

Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula 

Dar es Salaam, 1 Novemba 2024; saa 7:00 mchana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI