Header Ads Widget

MAKOBA : WAANDISHI WA HABARI NI NGUZO MUHIMU KUILINDA AMANI YA TAIFA.


NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA

ALIYEKUWA Msemaji Mkuu wa Serikali, Balozi Tobiasi Makoba, amekabidhi rasmi ofisi kwa Katibu Mkuu na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, katika hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa makabidhiano hayo, Balozi Makoba alieleza shukrani zake kwa nafasi aliyopewa kuwatumikia wananchi, akisema amejifunza mengi kuhusu uwazi na uwajibikaji kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan. 

"Rais Samia amenifundisha umuhimu wa kuisemea serikali kwa uwazi na uwajibikaji, hatua ambayo imenifikisha kwenye uteuzi wa kuwa balozi," alisema Makoba.

Makoba amewahimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao kwa hekima ili kuimarisha utulivu wa nchi.


 "Waandishi wa habari wana nguvu kubwa ya kuleta utulivu au taharuki Tuendelee kutumia kalamu zetu kwa manufaa ya nchi yetu," amesisitiza.




Kwa upande wake, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa kuwaamini vijana na kuwapa nafasi za uongozi, akibainisha kuwa uteuzi wa kwake na wa Makoba ni mfano wa kuigwa.

 "Kwa niaba ya vijana wenzangu, tunamshukuru Rais kwa kutuamini. Kazi yetu sasa ni kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidii ili tusije kuwa 'vijana wa hovyo,'" amesema Msigwa.

Msigwa pia amewataka waandishi wa habari kushirikiana kwa karibu na serikali katika kulinda amani na kuhamasisha maendeleo. 

"Waandishi wa habari ni nguzo muhimu katika kulinda utulivu na maendeleo ya taifa. Tuendelee kuisaidia serikali ya Rais Dkt Samia  Suluhu Hassan kwa juhudi za pamoja," amesema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI