Header Ads Widget

MAKAMU MKUU WA CHUO IRINGA PROF EDWARD HOSEAH MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO


NA ZUHURA ZUKHERY MATUKIO DAIMA, IRINGA

Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dakt Philip Isdor Mpango  ameitaka wizara ya afya kushirikiana na chuo kikuu cha Iringa UoI katika kufanikisha kwa suala la uanzishwaji wa taaluma ya uuguzi na ukunga katika chuo kikuu cha Iringa 

Hayo aliyasema leo  december 13 mwaka huu alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 27 ya chuo kikuu cha Iringa (UoI) na kusema kuwa changamoto ya uhaba wawatumishi katika sekta ya afya bado ipo hapa nchini hivyo uanzishwaji wa kozi hiyo itasaidia kutatua changamoto iliyopo.


Alisema kuwa tanzania bado inakabiliwa na vifo vya mama na mtoto hivyo kuanzishwa kwa kozi ya uuguzi na ukunga katika chuo kikuu cha Iringa kutasaidia kuongeza watumishi wabobezi katika sekta hiyo jambo litakalotatua changamoto hiyo.

“Tanzania bado tunakabiliwa na changamoto ya vifo vitokanavyo na mama na mtoto kwa baadhi ya maeneo japo tumepiga hatua kubwa katika kukabiliana nayo hiyo changamoto lakini bado kuna maeneo tatizo lipo hivyo niwapongeze kwa mpango wenu huo wa kuanzisha kozi ya ukunga na uuguzi, na muagiza waziri wa afya ashirikiane na chuo hicho kuona mambo yanayotokana na serikali yanafanyiwa kazi haraka ili kozi hiyo ianze.” alisema Dkt Mpango.


Aidha dkt Mpango ameiagiza tarura chini ya tamisemi kutenga bajeti ya ujenzi wa barabara inayoelekea chuoni hapo ikitokea barabara kuu ya Dodoma kutokana na miundombinu ya barabara hiyo 

Alisema kuwa ifikapo mwaka ujao wa fedha barabara hiyo ianze kutenengenezwa kwa kiwango cha lami ili kuondokana na changamoto ya ubovu wa barabara zilizozunguka chuo hicho.

Akizungumzia taaluma makamo wa Rais Dkt Mpango aliwataka wahitimu kuacha kukimbilia mafanikio ya haraka bali wajitume katika kufanya kazi itakayowaletea mafanikio 

Wahitimu niwasihi acheni tamaa ya kukimbilia mafanikio ya haraka fanyeni kazi kwa bidii na kwa ufanisi mafanikio yatakuja na msiache kujiendeleza kitaaluma mnapopata nafasi ya kusoma someni ili kujiimarisha kitaaluma lakini kikazi na uchumi wenu utakua kwa haraka kuliko mkipita njia za mkato” alisema dkt Mpango.

Alisema kuwa taasisi binafsi zione haja ya kushirikiana na vyuo vikuu vya serikali kufadhili tafiti mbambali zitakazowasaidia kuongeza ufanisi kwa wanafunzi ambao baadae watakuwa na uwezo wa kujiajiri.


Awali Makamu mkuu wa chuo kikuu cha iringa profesa  Edward  Hoseah alisema chuo hicho kinampango wakuanzisha kozi ya unesi na ukunga ili kukabiliana na uhaba wa watumishi wa sekta ya afya.

Alisema kuwa wanatarajia kuanzisha kozi ya uuguzi na ukunga mapema baada ya kupata baraka kutoka serikalini pamoja na kukalika kwa baadhi ya mambo ambayo yapochini ya wizara ya afya

Alisema sekta ya afya ni sekta inayotakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee kwa kuwa ndio sekta iliyobeba uhai wa mwanadamu.

Aidha alisema kuwa chuo hicho kinatambua hamasa inayofanywa na serikali juu ya matumizi ya nishati safi hivyo chuo kimepanda miti 1900 Kilolo na miti 500 kuzunguka chuo hicho.


Mh. Mgeni rasmi tumekuwa tukipamba na uharibifu wa mazingira kwa kupanda miti maeneo mbalimbali ili kurudisha uoto wa asili lakini bado kuna watanzania wanajenga nyumba juu ya milima hii ni changamoto kubwa sana.” alisema profesa Hosea.


Katika mahafali hayo mkuu wa chuo kikuu cha iringa ambaye pia ni mkuu wa majeshi mstaafu Venance Mabeo amewatunuku wahitimu 1751 wa ngazi mbalimbali katika chuo hicho  huku makamu Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzani Philip Isidor Mpango akitunukiwa tuzo maalum ya chuo hicho ya utunzaji wa mazingira na mkuu wa majeshi nchini jenelali Jacob Mkunda akitunukiwa tuzo maalum ya chuo kikuu cha Iringa kwa jitihada za kuimarisha uhusiano kati ya majeshi na chuo cha Iringa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI