Header Ads Widget

KUTEKWA KWA ABDUL NONDO ,THRDC WATOA TAMKO ZITO KULAANI MATUKIO YA UTEKAJI NCHINI

 


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kimelaani matukio ya utekaji yanayoendelea hapa nchini, ikiwa ni saa chache baada ya taarifa zilizotolewa na chama cha ACT- Wazalendo na Jeshi la polisi juu ya madai ya kutekwa kwa  Kiongozi wa Ngome ya vijana wa chama cha ACT @ACTwazalendo , Abdul Nondo katika eneo la kituo cha mabasi Magufuli, Dar es salaam.

Akizungumzia suala hilo, Mratibu Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa  amesema mtandao huo unasikitishwa na tukio hilo pamoja na mengine ambayo yamewahi kutokea huko nyuma kwani vyombo vya usalama mpaka sasa havitoi taarifa za ufuatiliaji juu ya matukio hayo ikiwepo suala la Tarimo na wengine.

Olengurumwa  amemuomba  Rais Samia Suluhu, kusikia kilio cha watetezi wa haki za binadamu juu ya uundwaji wa tume huru ya kuchunguza matukio hayo kwani yanatia doa Taifa.

"Tunaomba mheshimiwa Rais aweze kuliingilia suala hili kwani kupotea kwa watu, ni maisha ya watu, hofu za watu kupotea zikizidi hazijengi Taifa. Ni muhumu sana kwa sasa kutumia ile falsafa ya 4R Katika mambo kama haya hasa ya utekaji, inaweza kutuvusha hapa na watu wakabakia kuwa salama.

Tunalaani na tunatoa rai kwa vyombo husika viweze kufuatilia kwa haraka suala hili ili kuweza kujua nini kimemtokea Bwana Nondo, na aweze kupatikana haraka." Amesema Olengurumwa

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI