Header Ads Widget

JAMII IELIMISHWE UMUHIMU WA MAZOEZI

 



Na Hadija Omary 

Imebainishwa kuwa bado Jamii ina mtazamo chanya juu ya uwepo wa vikundi vya jogging club zinazojihusisha na mazoezi Katika Maeneo tofauti hapa Nchini ikihusisha vikundi hivyo na makundi ya wahuni


Akizungumza kwa niaba ya katibu wa Waziri wa kilimo Ally mngwali wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya jogging club ya Sobibo jogging klabu iliyopo Katika Kata ya Songosongo Wilaya Kilwa Mkoani Lindi bwana Alubeya kilambo Amesema dhana hiyo haina mashiko


Katika bonanza Hilo kililowakutanisha wanamichezo zaidi ya 400 kutoka Katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro, Dar es salaam na Zanzibar lilihusisha mazoezi ya viungo pamoja na mbio za kilometa 8


Kilambo Amesema bado wananchi wanapaswa kutambua kuwa kuna Umuhimu mkubwa kuwepo kwa vikundi hivyo vya jogging kwani vimekuwa vikisaidia Hata kuhamasisha shughuli mbalimbali za kiserikali 


" Nimeambiwa hapa Songosongo pia wapo Watu ambao bado hawajaelewa Umuhimu wa vilabu hivyo na Hata shughuli wanazozifanya niwatake viongozi kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi na Mimi naahidi pale mtakapokuwa tayari kufanya mikutano ya uhamasishaji Mimi nipo tayari kugharamia mikutano hiyo"


"Hata hivyo Katika kuunga mkono vilabu hivyo kilambo ameahidi kuvisapoti vilabu vyote vilivyoshiriki bonanza Hilo vifaa vya uchunguzi wa Afya vitakavyowasaidia kufahamu Afya zao kabla ya kufanya mazoezi"


Awali akisoma lisala ya klabu hiyo Katibu wa Sobibo jogging bwana Maliki Mzee Amesema alieleza namna ambavyo Jamii hiyo isivyoona Umuhimu wa uwepo wa vilabu hivyo ya jogging licha ya kujihususha na kushiriki Katika maswala mbalimbali ya kijamii ikiwa pamoja na usafi wa mazingira Katika fukwe za bahari


Diwani wa Kata hiyo ya Songosongo Hassan Swalehe alitumia fursa hiyo kuwashukuru wanamichezo wote waliojitokeza kwa wingi kushiriki bonanza Hilo huku Afisa kutoka shirika la Maendeleo ya petrol Tanzania TPDC Bwana  JACOB akiwahamasisha wanamichezo kuwa mabarozi Katika kulinda miundombinu hiyo ya gesi


Baadhi ya wanamichezo walioshiriki Bonanza Hilo wamesema kupitia mabonaza hayo wanaweza kujifunza na kupata fursa mpya kutoka kwa Watu wengine


" Mabonaza haya yamekuwa msaada mkubwa kwa Sisi wanavilabu kwani mkusanyiko huu unahusisha Watu wengi na kutoka Maeneo tofauti tofauti wapo wafanya Biashara, wapo wavuvi, wajasiliamali na Hata watumishi wa Serikali" alisema Hadija Mohame

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI