Header Ads Widget

DKT BITEKO ASHIRIKI KUAGA MWILI WA DKT NDUNGULILE

 





Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Disemba 2, 2024 ameshiriki Misa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Dkt. Ndugulile na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI