Rukwa Matukio Daima App
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Leo Disemba,04,2024 amepokea Kompyuta moja ya kuhifadhia data sanjari na kuwashukru wadau wa mazingira waliokuwa wakitekeleza mradi katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi katika vijiji saba vya ikiwemo Kijiji cha Tambaruka, Lyele na Kisula n.k.
Hayo yamejili kwenye kikao cha kuhitimisha mradi wa Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) na Shirika la Maendeleo Endelevu Rukwa ( RUSUDEO) kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Rukwa.
Kwa upande Msimamizi wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili Bi. Hana Lupembe amsema mradi huo wa miaka mitano ulianza mwaka 2020 hadi 2025 umenufaisha vijiji 18 katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga.
Mratibu huyo ametaja mafanikio mengine ni pamoja na kuwezesha halmashauri utengaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 13 kati ya 18 sawa na asilimia 86 ya lengo na pia wametoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi 2,170 kati ya lengo la kuwafikia watu 1,798.
Mradi huo wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili ulikuwa unatekelezwa na LEAT pamoja na RUSUDEO kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani ( USAID.
0 Comments