Header Ads Widget

BAKWATA KIGOMA WATOA NENO KUHUSU MIRADI,KUPOROMOKA KWA MAADILI


 Na Fadhili Abdallah,Kigoma

HALMASHAURI Kuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoa Kigoma na Baraza la Masheikh la baraza hilo mkoani Kigoma wamefanya mkutano Mkuu maalum kuJadili utekelezaji wa miradi na kuporomoka kwa maadili kwa viongozi na waumini wa dini hiyo mkoani humo.

Shekhe wa mkoa Kigoma, Hassan Iddi Kiburwa akizungumza mbele ya waandishi wa Habari wakati wa kikao hicho alisema kuwa mambo mawili makubwa ndiyo ajenda kuu ya kikao hicho kilichowakutanisha wajumbe wa Halmashauri kuu ya mkoa na wajumbe wa baraza la Mashekhe ambayo yamekuwa na changamoto hivyo wajumbe hao watajadili naona ya kuyashughulikia mambo hayo.

Kiburwa alisema kuwa uongozi wa wilaya wa baraza hilo umekuwa ukianzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi lakini ikiwemo elimu,afya, kilimo na masuala mengine ya kijamii lakini miradi mingi bado inasuasua kwa sababu hakuna mkazo na mikakati ya Pamoja hivyo kikao hicho kitajadili na kutoka na azimio.

Kuhusu kuporomoka kwa maadili ya baadhi ya viongozi na waumini alisema kuwa itakuwa pia ni ajenda kutokana na kuwepo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya nafasi ya baadhi ya viongozi na mashekhe ambao ndiyo msingi wa maadili ya jamii hivyo tuhuma hizo zinaathiri pia maadili ya jamii.

Akizungumza kuhusu mkutano huo Mjumbe wa Halmashauri ya baraza la BAKWATA mkoa akitokea wilaya ya Kasulu, Ruheta Ahmad Hussein alisema kuwa mkutano huo ni muhimu kwao ili kujadili kukwama kwa mradi wa mkoa wa kituo cha afya baada ya kusuasua kwa michango lakini kushindwa kupata wafadhili na wahisani kumalizia mradi huo.

 Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Mashekhe mkoa Kigoma, Haji Maulid Msangi alisema kuwa zipo taarifa za vitendo visivyo vya kimaadili vinavyofanywa na baadhi ya mashekhe na waumini wa kiislam hivyo kikao hicho pia kitatumia nafasi hiyo kuzungumza, kujadili na kutoa na maazimio ya nini kifanyike.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI