Na Fadhili Abdallah,Kigoma
KIONGOZI wa Chama Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa hawaridhishwi na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa uliofanyika November 27 mwakaa huu hivyo wameita serikali kutangaza kuwa uchaguzi huo batili na ufanyike upya.
Zitto alisema hayo Juzi jioni akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kawawa Ujiji Mjini Kigoma na kueleza kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki hivyo wananchama wa chama hicho kutowapa ushirikiano viongozi hao wa mitaa waliochaguliwa.
Kutokana na matokeo yaliyotokea Zitto amemtaka Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Mohamed Mchengerwa kuitisha uchaguzi mwingune ambao ni huru na wa haki ambao utawapa nafasi vyama vyote vya siasa na wagombea wao kushiriki kwa uhuru bila kuwepo kwa hila ambazo zinachangia baadhi ya vyama kupoteza ushindi wao.
Sambamba na hilo Kiongozi huyo Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo alisema kuwa chama hicho kimepangaa kufungua kesi kumshitaki Mkurugenzi wa manispaa na wenyeviti wa mitaa 67 kati ya 68 akitaka ushindi wao utenguliwe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Chama cha ACT Wazalendo, Muhonga Ruhwanya amemtaka Waziri Mchengerwa kutangaza upya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani huu uliotangazwa matokeo yake ni batili.
Ruwahnya alisema kuwa ili kuinusuru nchi na ubaguzi unaotakana na matokeo ya uchaguzi huo ni vizuri uchaguzi ukatangazwa upya na ufanyike baada ya kufanyika kwa marekebisho ya katiba

.jpg)





0 Comments