Header Ads Widget

WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA YA NKINGA WAHIMIZWA KUFANYAKAZI KWA MIIKO NA MAADILI YA TAALUMA ZAO.

Na Lubango Mashauri, Matukio Daima App Igunga. 

WAUGUZI na Madaktari tarajali katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyopo kijiji ncha Nkinga Kata ya Nkinga Wilayini Igunga, wamehimizwa kufanyakazi kwa miiko na maadili ya taaluma zao ili kuendana na sera na maono ya taasisi hiyo. 

Hayo yamebainishwa na Mganga Mfawidhi Dkt.Tito Chaula katika mafunzo maalumu yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili kuzifahamu sera na tunu za taasisi.

Amesema kuwa, kila taasisi inapoanzishwa inakuwa na kusudi la kuanzishwa kwake, ni vema watumishi wapya wanapoingia kazini kufahamu maono na sera za taasisi husika.

"Hospitali hii imejengwa katika misingi ya Kikristo yenye kumjali mgonjwa kwanza, kwetu sisi mgonjwa ni namba moja na tunahudumia wagonjwa wa aina zote bila kujali hali zao"

"Hatutegemei kusikia kati yenu kuna mtumishi ameletwa ofisini kwa swala la kimaadili, fanyeni kazi kwa maadili na miiko ya taaluma zenu huku mkimtanguliza Mungu kwanza" akisema Dkt.Chaula 

Aidha, Dkt.Chaula ameendelea kwa kusema kuwa, Hospitali sio majengo bali ni watoa huduma na wateja (wagonjwa) hivyo kila mtumishi akifanyakazi kwa kujitoa watayafikia malengo ya taasisi kwa pamoja.

Ameongeza, kila mmoja anapaswa kumuona mwenzake kuwa bora kwakuwa wanafanya kazi kwa kutegemeana kwani Hospitali ya Rufaa ya Nkinga inafanyakazi katika umoja (Team Work).

Amemaliza kusema kwa kuwahimiza watumishi hao kuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano unaofuata hatua ya kiuongozi katika kufikisha taarifa zao.

Huku, Katibu wa Hospitali hiyo Leah Kagine amewahimiza watumishi hao kufuata kanuni na miongozo ya kazi katika kipindi chote cha mafunzo.

Kwa upande wake mratibu wa zoezi hilo Dkt.Jacqueline Suba amewakumbusha watumishi hao kutumia vema mfumo wa kumbukumbuza za taarifa za mgonjwa uliowekwa na taasisi.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI