waziri wa TAMISEMI Mhe Mchengerwa
NA MATUKIODAIMA APP, ITILIMA
WAKULIMA waliosomba vifaa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Mwaswale Kata ya Mwaswale, Tarafa ya Bumela katika Halmashauri ya Itilima mkoani Simiyu wameilalamikia halmashauri hiyo kwa kushindwa kuwalipa fedha zao zaidi ya Shilingi milioni 7 baada ya kufanya kazi ya kusomba vifaa vya ujenzi wa shule mpya ya Mwaswale wilayani humo.
WAKULIMA waliosomba vifaa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Mwaswale Kata ya Mwaswale, Tarafa ya Bumela katika Halmashauri ya Itilima mkoani Simiyu wameilalamikia halmashauri hiyo kwa kushindwa kuwalipa fedha zao zaidi ya Shilingi milioni 7 baada ya kufanya kazi ya kusomba vifaa vya ujenzi wa shule mpya ya Mwaswale wilayani humo.
Wakulima hao ambao walitumia trekta zao kufanya kazi ya kusomba mawe, kokoto, mchanga na vifaa vingine wamemuomba Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengelwa kuingilia kati suala hilo ili waweze kulipwa fedha zao hizo.
Kwa nyakati tofauti wakulima hao ambao wamedai wanamiliki trekta za mikopo ya benki, walisema walipewa tenda ya kusomba vifaa mbalimbali vya ujenzi mwaka jana 2023, lakini tangu wakati huo wamekuwa wakipigwa danadana kuhusu malipo yao na kuwasababishia mitaji yao kuyumba.
Mmoja wa wakulima hao, Elias Musingi alisema yeye peke yake anadai jumla ya Shilingi milioni 3,375,000 kutokana na kusomba vifaa mbalimbali na kufikisha tripu 75 kwa kutumia trekta yake.
Musingi alisema walipewa mikataba ya kusomba mawe, kokoto, nondo, mchanga na vifaa vingine vilivyokuwa vimehifadhiwa kwenye majengo ya shule ya zamani, Mwaswale na kuvipeleka eneo ilipojengwa shule mpya ya msingi yenye jina hilo hilo la Mwaswale.
Pamoja na mambo mengine alionyesha mkataba wenye saini ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Jilala Mboje.
Alisema awali walikubaliana kila tripu moja kulipwa Shilingi 45,000 bila kujali aina ya vifaa.
Kwenye mkataba huo walikubaliana wangelipwa ndani ya wiki mbili baada ya kukamilisha kazi hiyo jambo ambalo halikutekelezwa kwani walipokea sehemu ya malipo ya awali tu na hawakuwahi kulipwa tena hadi sasa.
"Ninao mkataba halisi tulioingia na aliyekuwa Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mwaswale, tulikubaliana watakuwa wanalipa kila tripu moja Sh 45,000, awali nilisomba tripu 100 nikalipwa tripu 50 tu. Baadaye niliongeza tripu 25, hivyo jumla ninadai tripu 75 sawa na Shilingi milioni 3, 375.
Wakulima wengine, Malulu Luplemi na Ndawele Tabi kwa upade wao wanadai zaidi ya Shilingi milioni 4, baada ya kufanyakazi ya kusomba vifaa mbalimbali vya ujenzi wa shule hiyo mpya ya Mwaswale.
Malulu alisema deni hilo limewasababishia usumbufu mkubwa kwani wanadaiwa na vibarua pamoja na wamiliki wa vituo vya mafuta walipokuwa wamekopa dizeli kwa ajili ya trekta.
"Deni lile mpaka sasa hatujui tumdai nani, kwakuwa mwalimu mkuu wa wakati huo alikwisha hamishwa, tumefuatilia kwa mkurugenzi wa halmashauri bila mafanikio, hivyo tunamuomba Waziri mwenye dhamana na TAMISEMI atusikie kilio chetu, hizi trekta tumezikopa tunadaiwa na mabenki, tunapata wakati mgumu, serikali itusaidie itulipe hizi fedha."alisema Malulu.
Aidha aliyekuwa Mwaimu Mkuu wa shule ya Mwaswale, Jilala Mboje alipoulizwa na kuhusu suala hilo, alikiri kuingia mkataba na wafanyabiashara hao, lakini alisema kila kitu kipo chini ya mkurugenzi wa halmashauri ya Itilima.
"Siwezi kusema kitu chochote, naomba umtafute mkurgenzi ndiye mwenye maneno yote kuhusu suala hilo"alisema Mboje.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima, Faraja Msigwa hakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Matuko Daima inaendela kumtafuta mkurugenzi huyo ili atolee ufaanuzi suala hilo.
mwisho
0 Comments