Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Viongozi wa dini mkoani Kigoma wametoa tamko wakitaka uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27 mwaka huu kufanyika kwa amani na utulivu huku wakitaka kila mdau wa uchaguzi kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria za uchaguzi zilizowekwa.
Viongozi hao wa dini wametoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika November 25 katika ofisi za Baraza Kuu la waislam (BAKWATA) Ujiji wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.
Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa Habari Askofu Mkuu wa wa kanisa la Pentekoste Motomoto (PMC),Ezra Utamya alisema kuwa wanamini uchaguzi utakuwa huru na haki kama kila mmoja atatimiza wajibu na majkumu yake kuufanya uchaguzi kufanya kwa amani.
Sambamba na hilo Askofu Utamya amewataka wasimamizi wa uchaguzi huo kutenda haki kwa kuwapa nafasi sawa wagombea wote huku akitaka mgombea aliyechaguliwa na wananchi na kushinda atangazwe.
Kwa upande wake Kaimu Shekhe wa BAKWATA wilaya Kigoma, Hassan Ally alisema kuwa wanaamini kwa mazingira ambayo serikali wameweka wanaamini uchaguzi wa amani iwapo kila mmoja atajichunga kwa ulimi wake na matendo yake kuepuka mambo ambayo yatachangia kuleta vurugu kwenye uchaguzi.
Kutokana na hilo ameomba Mwenyezi Mungu ajaalie uchaguzi huo uwe wa amani kwa kila mshikiri kupiga kura na wale ambao wananchi wamewachagua kwa kura nyingi wapewe nafasi ya kuwatumikia wananchi.
Miseke Shaban Maranda ni Mwananchi wa Ujiji katika manispaa ya Kigoma Ujiji alisema kuwa anaamini uchaguzi utaenda vizuri lakini ametaka viongozi wa vyama vya siasa na wapenzi wao wapige kura kwa amani na kurudi nyumbani badala ya kukaa kwenye vituo kwa madai ya kusubiri matokeo.
Mwisho.
0 Comments