Header Ads Widget

TAMISEMI YAWANOA JUMIKITA

 


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp, Dar


Jumuiya ya la Waandishi wa Mtandaoni  Tanzania (JUMIKITA)  wameshauriwa  kuzingatia weledi ,maadili, katika kuandika habari kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  ili kusaidia kutoa taarifa za uhakika na zenye ukweli kwa wananchi kuepuka kuleta  taharuki ndani ya Jamii.


Rai hiyo imetolewa leo Novemba 13, 2024 Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt Grace Maghembe. akifungua semina ya siku moja kwa Jumuiya ya waandishi wa habari za mtandaoni (JUMIKITA) Tanzania inaelekea katika tukio kubwa la uchaguzi wa Serikali za mitaa hivyo ni vyema waandishi kutumia Kalamu zao vizuri wanaporipoti taarifa za uchaguzi huo unaotarajiwa kuanza Novemba 27 mwaka huu .


" Tumeamua kutoa mafunzo haya yanayoendana na tukio kubwa la ambalo wananchi wanaokwenda kufanya maamuzi nani awaongoze Kwa miaka mitano na  lengo la Serikali ni kuona uchaguzi huo unakua huru na haki, hivyo ni vyema kwa waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli ili kuweka utulivu na amani ndani ya nchi" amesema Dr Magembe


Sanjari n hayo , amewashauri wananchi kuwapima viongozi wanaowachagua kwa hoja zenye maslahi mapana ya nchini na sio kuchagua viongozi ambao hawawezi kuwajibika kuwaletea maendeo ndani ya mitaa yao.


Dr Magembe ameshauri Mamlaka taasisi za Serikali  kutambua umuhimu wa waandishi wa habari wanapokua kwenye majukumu yao kwa kuwapatia vitambulisho maalumu ili kuepuka changamoto ambazo zinakua zinajitokeza ikiwemo vurugu.



Naye, Afisa Sheria wa Tamisemi Mihayo Kidete amesema kanuni ya Tanzania  ili mtu aweze kupata nafasi ya kugombea nafasi yoyote ni lazima awe kuanzia umri wa miaka 21 na awe amejindikisha katika daftari la mpiga kura na kutimiza masharti yote yaliowekwa katika kanuni za uchaguzi.


"Mtu hatakua na sifa za kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi endapo ataajiriwa au kuteuliwa katika wadhifu wowote katika utumishi wa umma au kuchaguliwa katika nafasi ya udiwani, ubunge, uspika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umakamu wa Rais au Rais wa nchi"amesema Mihayo.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumikita Shaban Matwebe ameshukuru  na ameipongeza Ofisi ya Rais tawala za Mikoa Tamisemi kwa kuona umuhimu wa kuwapa elimu wanahabari za mtandaoni kwani ulimwengu wa sasa ni wakidigital wanaofitiliwa sanaa poote mtu alio kupitia simu anajua nini kinaendelea.


Matwebe amesema  wanamitandao ya Kijamii ni  wanahabari, ambao wanatembea na vifaa vyao mkononi hufanya kazi popote walipo hivyo  amewahakikishia Tamisemi  baada ya semina hiyo wataona mabadiliko makubwa  taarifa zenye weledi na wananchi watajua  kanuni za uchaguzi .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI