Na Matukio Daima media
KIJANA Shalom Robert, mmoja wa vijana wanaoonyesha uzalendo na uhamasishaji wa maendeleo ndani ya jamii, amesisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika kuchangia maendeleo ya taifa pamoja na kushiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza na Matukio Daima media kuhusu jukumu la vijana, Shalom ambae kitaaluma ni mwandishi wa habari alieleza kuwa mchango wa vijana ni mkubwa mno, na jukumu lao la msingi ni kuendelea kuelimishana ili wasiyumbishwe na changamoto za kijamii na kisiasa.
“Kila mmoja anaona kazi zinazofanywa na serikali yetu chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tunajivunia sana maendeleo haya. Ni jukumu letu vijana kuhakikisha tunamuunga mkono Rais wetu kwa nguvu zote. Tukutane Novemba 27 tuchague viongozi bora,” alisema Shalom kwa msisitizo.
Shalom alitoa pongezi kwa serikali kwa juhudi kubwa za kuwainua vijana kiuchumi kupitia mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri mbalimbali nchini.
Kuwa mikopo hii imekuwa chachu ya maendeleo kwa vijana kwa kuwa imeongeza mitaji yao na kusaidia kuboresha maisha yao binafsi pamoja na familia zao
“Mikopo hii ikitumiwa vizuri na kurejeshwa kwa wakati, itapanua wigo wa fursa kwa vijana wengine. Ni muhimu kwa vijana kuhakikisha kuwa wanafuata masharti ya mikopo hii ili tuweze kuendelea kufaidika nayo na kuboresha uchumi wetu,” aliongeza.
Alisema kuwa kupitia mikopo hii, vijana wengi wameweza kuanzisha miradi midogo na ya kati, ikiwemo kilimo, biashara ndogondogo, na ufundi.
Alipongeza kuwa ajira na kupunguza changamoto za kiuchumi zinazowakumba vijana wengi vijijini na mijini.
Aidha Shalom alitaka vijana kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia kwa nguvu zote.
Alisisitiza kuwa maendeleo makubwa yanayoshuhudiwa nchini ni matokeo ya uongozi thabiti na maono ya Rais.
Alitoa wito kwa vijana kuwa mabalozi wa amani na maendeleo kwa kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania.
Alisema chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu, upatikanaji wa maji safi, na huduma za afya.
"Hii ni pamoja na maboresho katika sekta ya elimu na ujenzi wa barabara za kisasa zinazorahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma"
Alisema kuwa vijana wamepewa nafasi muhimu katika kufanikisha maendeleo haya kupitia programu mbalimbali zinazolenga kuwainua kiuchumi na kielimu.
Shalom alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila kijana kushiriki kikamilifu kuhakikisha kuwa mafanikio haya yanaendelea kudumu.
Kuhusu Uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji Shalom aliwahimiza vijana na wananchi kwa ujumla kufika kwenye uchaguzi wa Novemba 27 na kuchagua viongozi bora watakaoshirikiana na Rais Dkt. Samia kuendeleza kazi nzuri zinazofanyika.
“Ni lazima tuhakikishe kuwa tunachagua viongozi wenye maono na dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwa taifa letu Vijana, ni wakati wetu kufanya maamuzi sahihi,” alisisitiza.
Alisema kuwa vijana wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii, na kwa kushirikiana na serikali, Tanzania itaendelea kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
0 Comments